Pages


Home » » SAKATA LA KUTOFUNGWA KWA HARUSI, KAMATI YANUIA KUMFIKISHA MZAZI WA BIBI HARUSI MAHAKAMANI.

SAKATA LA KUTOFUNGWA KWA HARUSI, KAMATI YANUIA KUMFIKISHA MZAZI WA BIBI HARUSI MAHAKAMANI.

Kamanga na Matukio | 05:46 | 0 comments
 Familia ya Bibi Harusi Ikupa Mwalukosya (29) katika picha ya pamoja nje ya nyumba yao siku moja baada ya harusi kutofungwa kutokana Ukata, uliopelekea Bwana harusi Mwalimu Gervas Shihamba Makambuya (29), kushindwa kutuma pesa kwa ajili ya nauli ya kumfirisha Bibi harusi pamoja na wapambe.
 Bibi harusi Ikupa Mwalukosya (kushoto) akiwa na Mchungaji Nelusigwe Ikuka Mwangosi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Jimbo la Mwakaleli, akimfariji bibi harusi baada ya bwana harusi kushindwa kutuma pesa kwa ajili ya usafiri.
 Bwana harusi Mwalimu Gervas Shihamba Makambuya.
******
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Kamati iliyokuwa ikishughulikia harubi ya Mwalimu Gervas Mwashihamba Makambuya (29), imeazimia kumfikisha mahakamani mzazi wa Bibi harusi, Daktari Akimu Mwalukosya wa Kijiji cha Mbigili Mwakaleli Wilaya ya Rungwe.

Tamko hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bwana Jeremia Mahenge maarufu kwa jina la Vamponji, katika Ukumbi wa Vamponji Aprili 3 mwaka huu akidai sababu iliyotolewa na mzazi wa bibi harusi ya kuwa bwana harusi hakutuma usafiri wa kumchukua binti yao haziridhishi, kwani wangepewa taarifa mapema.

Mbali na hilo amesema wamesikitishwa na kitendo cha mshenga wa bwana harusi kwa kuwasaliti kwani hakuonekana siku ya alhamisi iliyopita huko kijijini kwao alipokuwa akiangwa binti Ikupa Akimu (29), kwa kile kilichotafsiriwa kuwa alirubuniwa na mzazi wa bibi harusi ili kuvuruga harusi hiyo.

Aidha katika Kikao hicho Bwana harusi Mwalimu Gervas ametoa tamko mbele ya wanakamati kuwa hayupo tayari kumwoa tena binti huyo, kutokana kitendo cha kushirikiana na mzazi inadhihirisha kuwa hakuwa na upendo wa dhati kwake.

Hata hivyo ameishukuru kamati ya maandalizi ya harusi yake kwa kitendo cha kiungwana walichokifanya na juhudi kubwa kutaka kufanikisha harusi hiyo lakini hali ikawa tete kutokana na wakwe zake kutokuwa radhi binti yao kuolewa naye.

Mwalimu Gervas ameongeza kuwa atawasiliana na washenga wake ili kurudishiwa mahali zake, huku kamati imepanga kuwasiliana na Mwanasheria kutokana na kitendo hicho ili kuangalia uwezekano wa kurejeshewa gharama zilizotumika kuandaa sherehe hiyo iliyo gharimu zaidi ya shilingi milioni 4,300,000.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger