Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Wadau wa zao la Kahawa kutoka Ukanda wa Nyanda za Juu wamelalamikia uteuzi wa Bodi ya wakurugenzi wa zao hilo nchini, iliyoteuliwa na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Profesa Jumanne Maghembe iliyoundwa Februari 8 mwaka huu itakayodumu kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe hiyo.
Wakiongea katika mikutano mbalimbali inayofanyika katika Kata zote zinazolima zao la kahawa Wilaya ya Mbozi ambazo ni pamoja na Nambizo, Itaka, Bara, Halungu, Msia, Igamba na Isansa.
Nyingine ni Ruanda, Iyula, Mlangali, Nyimbili, Isandula na Ihanda ambapo wakulima hao wamesema kuwa Mikoa ya Nyanda za Juu haina wawakilishi licha ya ukanda huu kuwa na mchango mkubwa wa uzalishaji wa zao hilo matharani Wilaya za Mbozi, Ileje, Rungwe na Mbeya Vijijini.
Mikutano hiyo inaendeshwa na Muungano wa Vikundi vya wakuliwa wa Kahawa, Wilaya ya Mbozi (MVIKAMBO) chini ya mwenyekiti wake Fredy Mgala, wakuliwa hao wamesema kuwa Bodi hiyo haikuzingatia kilio chao ikiwa ni pamoja na makampuni makubwa kununua kahawa mbichi na kuwanyonya wakulima na kwa mpango huo wakulima wa wilaya ya hiyo wamekuwa wakiyumbishwa hali inayopelekea ukusanyaji wa kahawa chafu licha ya kahawa yao kupendwa katika soko la kimataifa.
Baadhi ya wajumbe waliuteuliwa kwenda ni pamoja na Bibi Eva Hawa Sinale, Bibi Fatma A Faraji, Bwana Novatus Henrico Tiigelerwa kutoka Karangwe Kanda ya Magharibi, Bwana Erick Ng’imario Katibu mkuu chama cha wanunuzi wa kahawa, Mh Yasinth Ndunguru Ngwatura mwakilishi wa wakulima kanda ya kusini, Bwana Meynard E. Swai kutoka Kanda ya Kaskazini, Profesa James Teri kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania (TACRI), Mh John Damiano Komba Mbunge Jimbo la Mbinga Magharibi na Eng. Meraji Omari Msuya mhandisi wa Hdrolojia kutoka Wizara ya maji.
Hata hivyo kwa mtazamo huo Mkoa wa Mbeya kwa ujumla unakosa mwakilishi wa dhati kuwawakilisha wakulima wa zao hilo katika Bodi ya Kahawa, na kwamba wanamuomba Waziri Profesa Maghembe kuwaangalia kwa jicho la huruma ili waondokane na kero ya kukosa pembejeo za zao, ambazo ni aghali mno.
0 comments:
Post a Comment