Pages


Home » » TAZIZO LA UPATIKANAJI WA NISHATI YA UMEME

TAZIZO LA UPATIKANAJI WA NISHATI YA UMEME

Kamanga na Matukio | 05:56 | 0 comments
Habari na Richard Mwafulilwa, Mbalizi.
Tatizo la upatikanaji wa huduma ya umeme linalowakabili baadhi ya wananchi wa Jiji la Mbeya linatarajia kupatiwa ufumbuzi mwishoni mwa wiki hili.

Hayo yamesemwa na Kaimu Meneja wa Tanesco Mkoani Mbeya Eng, Julius Sabu wakati akizungumza na mwandishi wetu kuhusiana na sababu za kutopatikana kwa nishati ya umee katika maeneo ya Mbalizi na Iyunga.

Amesema taizo linapatiwa ufumbuzi baada ya kupatikana kwa transfoma ambazo shirika hilo tayari limetuma magari katika makao makuu Jijini Dar Es Salaam ili kuzichukua na kumaliza tatizo hilo.

Ameongeza kuwa tatizo kubwa linalochangia kutopatikana kwa nishati hiyo kwa baadhi ya maeneo jijini Mbeyana kutokana na wizi wa mafuta ambao umekithiri kwa kiasi kikubwa.

Eng, Sabu amewatakawananchi kutoa ushirikiano kwa shirika hilo uli kudhibiti wizi  huo ambao unachangia kuzorota kwa huduma hiyo.

hata hivyo amesema kuwa mtu yeyote atakayepatikana na transfoma, atakamatwa bila kusamehewa na mtu yeyote anayedaia kutengeneza transfoma kwa madai kuwa ni mfanyakazi wa Tanesco, anatakiwa kutoa kitambulisho vinginevyo akamatwe na kutoa taarifa kwa shirika hilo kwa njia ya simu.

Wakati huo ho amewaasa watu wote wanaotumia mafuta ya Transfoma kama mafuta ya kula waache mara moja kutokana na kusababisha kansa na magonjwa mengine.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger