Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Waziri
Mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Edward Ngoyai Lowassa
ametoa shilingi milioni 10, kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa la EAGT
lililopo Mji mdogo wa Tunduma, Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya.
Fedha
hizo zimetolewa jana katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa
hilo, iliyofanyika katika viwanja vya Hoteli ya High Class mjini humo.
Lowasa
alitumia zaidi ya dakika 28 pekee kuwepo kwenye viwanja hivyo ambapo
amesema kuwa watanazania wanapaswa kuwa na wito wa kujenga nyumba za
kuabudu kuliko kujenga zaidi nyumba za starehe zikiwemo Bar.
Amesema
kuwa amefurahi kualikwa katika harambee hiyo na kwamba kwa sasa nchi
ipo kwenye kipindi kigumu cha uchumi na masuala ya katiba mpya, hivyo
amewaomba wakristo kupanga ratiba ya kuiombea nchi ili iendelee kuwa na
amani na watanzania kuendelea kuimarisha ushirikiano na umoja wa kitaifa
uliopo nchini.
Aidha,
amesema jambo hilo ni muhimu kwa kila mtanzania akiliombea taifa,
Tanzania haitaweza kutokea migogoro na vita za wenyewe kwa wenyewe kama
ilivyo kwa mataifa mengine mfano Nigeria.
Baada
ya hotuba yake hiyo fupi aliwaita wasaidizi wake jukwaani na kuwaagiza
wampande na mfuko wa fedha na kisha akamkabidhi mfuko wa pesa taslimu
shilingiu milioni 10, Askofu Keneth Kasanga wa kanisa hilo.
Kwa
uapnde wake Askofu huyo alimshukuru Waziri mstaafu Lowasa ambaye ni
Mbunge wa Jimbo la Monduli kuwa amejenga nyumba ya Mungu na hawezi
kumuacha katika mambo yake yote na mahitaji pia.
Kanisa
hilo lina zaidi ya waumini 750, walipanga kuwa na kiasi cha shilingi
milioni 750 na siku hiyo zimekusanywa jumla ya shilingi milioni 17.9,
huku fedha zilizoahidiwa ni shilingi milioni 15.
0 comments:
Post a Comment