Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Wimbi la
kujichukulia sheria mkononi kwa wananchi pindi akamatwapo mhalifu
limezidi kushika kasi mkoani Mbeya, baada ya wananchi wanaojiita wenye
hasira kali kufanya mauaji, pasipo kumfikisha katika vyombo vya dola
kuchukuliwa hatua za kisheria.
Tukio
hilo limetokea Aprili 24 mwaka huu katika Mtaa wa Airpot Ilembo, Kata ya
Iyela Jijini Mbeya ambapo majira ya saa 12 kamili asubuhi, wananchi hao
walimuua Simon Samson (34) kwa kutumia vitu vyenye ncha kali sehemu
mbalimbali za mwili wake na kusababisha kifo chake papohapo.
Baada ya mauaji hao wananchi hao waliuchukua mwili wa marehemu na kuutupia katika korongo lililopo mtaa wa Iyela .
Aidha wananchi hao wamemtuhumu marehemu kuwa ni mwizi katika mtaa huo, ingawa hakukutwa na kitu chochote wakati wa tukio hilo.
Mpaka
hivi sasa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusika na mauaji hayo hali
mwili wa marehemu ukiwa umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Jijini
hapa.
Wakati
huo huo mtu asiyefahamika jina wala makazi ameokotwa akiwa amefariki na
mwili wake kutupwa kando kando ya mto Mita karibu na makaburi ya
Sabasaba jijini hapa na mpaka sasa mwili hakujaweza kutambuliwa.
Kaimu
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya Barakiel Masaki amethibitisha
kutokea kwa matukio yote mawili na kwamba uchunguzi unafanyika ili
kuweza kubaini watuhumiwa.
0 comments:
Post a Comment