Habari na Mwandishi maalumu, Mbeya.
Benki ya damu Kanda ya Nyanda za Juu Kusini
inakabiliwa na upungufu mkubwa wa damu hali ambayo inahatarisha usalama wa
maisha hasa kwa akina mama wajawazito na wagonjwa wanatokanao na ajali ambao
wamekuwa wakihitaji damu kwa wingi.
Akiongea na mwandishi wetu ofisini kwake meneja wa
benki kuu ya kuchangia damu kanda ya nyanda za juu kusini dokta Baliyima Lelo amesema
kuwa benki hiyo inaupungufu wa chupa mia moja za damu salama.
Amesema benki hiyo huitaji chupa mia tatu kila siku
za damu salama lakini kwa sasa benki hiyo ambayo husambaza damu katika
hospitali zote za mikoa ya kanda ya nyanda za juu kusini imekuwa ikipata lita
200 za damu salama badala ya mia tatu.
Kutokana na tatizo hilo Dokta Lelo ameiomba jamii kuchangia damu
ili kusaidia kuokoa maisha kwa wagonjwa wenye uhitaji mkubwa wa damu hasa kwa
akina mama wajawazito ambao mara nyingi wamekuwa wakionekana kuwa na upungufu
wa damu mwilini.
0 comments:
Post a Comment