Habari na Baraka Lusajo, Mbeya.
Katika hali isiyo ya kawaida wazee wa kimilia Mkoani Mbeya, wamefanikiwa kulinasa jini katika eneo la Iyunga, Kata ya Swaya jijini Mbeya, Aprili 15 mwaka huu majira ya saa nne asubuhi.
Wazee hao wamedai kuwa jini hilo lililofahamika kwa jina la Mwanahawa Saidi likiwa limetokea Tegeta jijini Dar es salaam na kuja mkoani hapa likiwa limeongozana na majini matano, ambayo ndiyo yamemtoa katika eneo linaloishi.
Kwa mujibu wa Jini hilo limedai kuwa na watoto wanane, ambapo watoto watatu wanaasili ya jini lakini watoto watano hawana asili hiyo, hivyo kutokana na hali hiyo watoto watatu huwa wanapotea hadi kufikia miezi mitatu na zaidi, baadaye hurejea makazini kwao.
Hata hivyo jinni hilo limesema dhumuni ya kuja Mbeya ni kupata maombezi kutoka kwa waganga wa jadi, ili kuweza kurudi katika hali ya ubinadamu, kutokana na kuwa na hali ya sura mbili kwa kubadilika badilika kila wakati.
Wakati huo huo Mwenyekiti wa Chama cha Muungano wa Jamii cha kupambana na maobu Mkoani hapa (MUJATA) Bwaba Soja Masoko, amewataka wananchi kuwa katika hali ya ujasiri pindi wanapokutana na mapepo kama haya, hivyoamelitaka jini hilo kurejeshwa Jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment