Pages


Home » » AUA KIKONGWE BAADA YA KUNYIMWA NOTO WA KUWASHIA SIGARA

AUA KIKONGWE BAADA YA KUNYIMWA NOTO WA KUWASHIA SIGARA

Kamanga na Matukio | 04:02 | 0 comments


 Kama wewe ni mvutaji wa sigara kupita kiasi/mtu ambaye katika mazingira yako unayoishi unakumbana na moshi wa sigara, basi utumiaji wa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha vitamin A kama papai, kutakuepusha na kupatwa na madhara yatokanayo na moshi wa sigara.
*****
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Bwana Benjamini Mwankita(28), mkazi wa Kijiji cha Masukulu, Wilaya ya Rungwe baada ya kutuhumiwa kumuua Lazaro Mwalwima(70) kwa kutumia kiwiko cha mkono.

Tukio hilo limetokea Aprili 9 Mwaka huu majira ya saa 12:30 jioni ambapo Benjamini alienda nyumbani kwa marehemu na kuomba moto wa kuwashia sigara, marehemu alipokataa ndipo alimpigwa kiwiko na kupoteza maisha.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Barakiel Masaki amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa amekamatwa na upelelezi wa tukio unaendelea.

Ameongeza kuwa mtu mmoja aitwaye Emmanuel Pater mkazi wa Kaloleni amefariki dunia baada ya gari alilokuwa akiliendesha kugonga mti na kufariki papo hapo.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 3:10 usiku katika eneo la Old Vwawa, barabara ya Mbeya/Tunduma ambapo gari hilo aina ya IT 6657 aina ya Toyota Sprinter liliacha njia kisha kugonga mti hali iliyompelekea dereva huyo kufikwa na mauti.

Hata hivyo chanzo cha ajali hiyo kimetajwa kuwa ni mwendokasi  na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger