Mbunge
wa Jimbo la Mbozi Magharibi Mheshimiwa David Silinde ambaye naye
akiwaasa wananchi kuwa watulivu ili kumsikiliza Makamu wa Rais na
kusahau yaliyotokea, ambaye anakuja kwa shughuli za Kiserikali na sio
kisiasa na kama kuna tatizo lolote basi ni muda muafaka wa kumuuliza
Makamu wa Rais ili kutafutiwa ufumbuzi.(Picha na Maktaba yetu).
*******
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbozi.
Wiki moja baada ya mfululizo wa
Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Jijini Mbeya kuachia nyadhifa zao kupitia
Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), wimbi hilo sasa limebeba sura mpya kwa kuhamia Wilaya ya
Mbozi.
Katika hali isiyo ya kawaida Aprili
25 mwaka huu mchumi wa CCM wilaya hiyo Bi Happiness Kwilabya aliachia
wadhifa huo na kujiunga na CHADEMA, akifuatana na wanachama 18 katika
mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Kata hiyo maarufu kama
uwanja wa malori wilayani hapo.
Wanachama hao walipokelewa na
Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya hiyo Bwana Joseph Mwachembe maarufu kama
China, ambaye pia Katibu wa Mbunge wa Mbozi Magharibi Mheshimiwa David
Silinde.
Akiongea katika mkutano huo
uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi ambao umevuta hisia za watu wengi
ambapo Bi Happiness amesema sababu kutoka CCM na kuhamia CHADEMA ni
kutokana na mipango mingi inayopangwa si ya utekelezaji na badala yake
wamekuwa wakijinufaisha wao binafsi na kuwafanya wananchi kuishi katika
hali ya umaskini.
Aidha amezungumzia kero mbalimbali
kuwa miradi mingi aliyokuwa akiibuni na kushauri kama mchumi imekuwa
ikikwamishwa na baadhi ya viongozi, ambao wapo kwa maslahi yao binafsi
na si chama wala taifa kwa ujumla.
Hata hivyo amesema hajashawishiwa na
mtu yeyote kukihama chama tawala na kwamba amehamia chama kingine ili
kuhakikisha anapigania haki na maslahi ya watanzania.
Kwa
takribani mwezi mmoja hivi sasa CCM imepoteza zaidi ya wenyeviti wa
mitaa wapatao watano, ambao wameamia CHADEMA na mwingine aliposimamishwa
kugombea wadhifa huo aliibuka na ushindi wa kishindo katika Mtaa wa
Nonde Bwana Ezekiel King, ambaye pia alishawahi kuwa golikipa wa Tukuyu
Stars na Mapinduzi Stars ya Mbeya, mtaa anaoishi Mstahiki Meya wa Jiji
la Mbeya Bwana Athanas Kapunga.
1 comments:
Watanzania wa mwanzo walikuwa ni wa s.l.p,lakini watanzania wa leo ni wa dot com.wanafuata misingi ya demokrasia,kama sehemu haina maslahi,haikuelewi,tafuta mahali utakapo ona panaeleweka nenda.Demokrasia hoyeee!.
Post a Comment