Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abass Kandoro akihimiza jambo wakati akiongea na waandishi wa habari ofini kwake.
*******
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbarali.
Wananchi wa Kijiji cha Ijumbi, Kata
ya Ruiwa Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya, wamemuomba Mkuu wa Mkoa Bwana
Abbas Kandoro kuingilia kati mgogoro baina ya pande mbili zinazopingana
Diwani na Afisa Mtendaji wa Kata wakidaiwa kumuengua Mwenyekiti wa
kijiji hicho kwa kutumia madaraka yao.
Kauli hiyo imetolewa na wananchi wa
Kata hiyo kawa nyakati tofauti wakati wakiongea na mtandao huu kijijini
hapo, ambapo inadaiwa Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bwana John Kalikumoyo
ameenguliwa uongozi kutokana na ubadhilifu pia kuitisha mikutano ya
hadhara bila kibali na kuzuia wananchi katika shughuli za maendeleo.
Wananchi hao wamepinga madai hayo na
kuwa ni njama za mtendaji Kata Bwana Jordan Masweve na Diwani mheshimiwa
Alex Mdimilage, kwani ya kudhoofisha juhudi za mwenyekiti huyo kwa
kuzuia mianya ya upatikanaji wa pesa kinyume na utaratibu wa makusanyo
ya pesa za serikali.
Imedaiwa kuwa Viongozi hao wa kata
waliitisha mkutano wa halmashauri ya Kijiji Aprili 17 mwaka huu,
wakimtuhumu Bwana Kalikumoyo kwamba ameuza ng'ombe aliyekamatwa kijijini
hapo na kujipatia fedha jumala ya shilingi milioni 1,080,000 na makosa
hayo yanafanya kupoteza sifa za kuwa kiongozi.
Aidha viongozi hao walimtaarifu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali na yeye kuandika barua
Aprili 18 mwaka huu, kutengua uongozi wa uenyekiti wa kijiji na
kumkaimisha Afisa Mtendaji wa Kijiji.
Katika sakata hilo wananchi wa kijiji
hicho wamemuomba Mkuu wa Mkoa Bwana Kandoro, kwenda haraka iwezekanavyo
kijijini hapo ili kuleta suluhu kwani wananchi hao wamedai kuwa
viongozi hao wa kata Bwana Masweve na Mdimilage ndio wabadhilifu.
Hata hivyo miongoni mwa vitendo
vinavyolalamikiwa na wanachi kwa viongozi hao ni pamoja na kujipatia
zaidi ya shilingi milioni 24 kutoka kwa wafugaji ambazo hazijaingia
katika mfuko wa kijiji, ba kwamba suala hili Mkuu wa mkoa anapaswa
kuunda tume ya kuchunguza kwani hawapo tayari kuchangia shughuli za
maendeleo kama vile ujenzi wa shule za sekondari, zahanati na maji.
Wakati huo huo wamesema sababu yao ya
kutka kususia kuchangia shughuli za maendeleo ni kutokana na viongozi
hao kukataa kusoma bajeti ya mapato na matumizi ya kijiji, na badala
yake kuwataka viongozi wa Vijiji kusoma taarifa hizo, hali
inayowapelekea kuwa na swali kuwa Serikali ya kata haina mapato na
matumizi?.
Baadhi ya vijiji vinavyohusishwa
kutumiwa na Viongozi hao wa kata ni Motomoto, Malamba, Mahango, Igalako
na Udindilwa vyote vilivyopo katika Kata ya Ruiwa.