Habari na Mtandao huu, Mbeya.
Wilaya ya Mbeya inakabiliwa na upungufu wa madarasa kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2012.
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Mbeya Evans Balama wakati akizungumza na bomba fm mwishoni mwa juma,balama amesema jiji la mbeya linakabiliwa na upungufu wa madarasa 59 wakati wilaya ya mbeya vijijini inakabiliwa na upungufu wa madarasa kumi na tano
Aidha Balama ameongeza kuwa wazazi wanawajibu wa kukamilisha madarasa hayo ili wanafunzi waweze kuanza masomo haraka iwezekanavyo ili ifikapo mwishoni mwa mwezi february madarasa hayo yawe yamekamilika ili wanafunzi waanze masomo haraka
Kwa upande wake afisa elimu mkoa wa mbeya Juma Kaponda amesema hawezi kutoa nafasi kwa wanafunzi ambao hawajapangiwa shule hadi watakapokamilisha ujenzi wa madarasa hayo huku akitolea mfano kwa kata ya iyela ina upungufu wa madarasa tisa na kusababisha zaidi ya wanafunzi 300 kukosa nafasi ya kupangiwa shule na hivyo kubaki nyumbani hadi sasa huku wenzao wakiendelea na masomo.
0 comments:
Post a Comment