Pages


Home » » KUIBIWA MSIMU WA SIKUKUU

KUIBIWA MSIMU WA SIKUKUU

Kamanga na Matukio | 09:13 | 0 comments
Habari na mtandao huu.
Dereva wa kampuni ya KTM inayaosafirisha mizigo kutoka nchini na kupeleka nchi za kusini mwa bara la Afrika, Bwana Hussein Bondoe Peter mwenyeji wa mkoa wa Tanga ambaye ni mkazi wa jijini Dar es salaam amemtelekeza mkewe aitaye Halima Swedi (28) mkazi wa Bunjumai nchini Kongo na mtoto wa kike Bahati Hussein (4).

Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Mpemba wilayani Mbozi baada ya dereva huyo kudai gari lake limeishiwa mafuta hivyo kumtuma mkewe aende Tunduma ambapo ni umbali wa kilomita 10 kutoka eneo ambalo linadaiwa gari hilo kishiwa mafuta, mara alipoondoka kwenda Tunduma mwanamke huyo dereva  aliondoka na kila kitu cha mke na mwanae.

Mwanamke huyo hakupewa pesa yoyote ya mafuta, hivyo alielekezwa mahali pakwenda kuzichukua pesa za matumizi na kuwepa shilingi laki moja.

Hata hivyo mpaka sasa dereva huyo hana mawasiliano yoyote na mwanamke huyo kwa takribani wiki moja sasa, hali inayopelekea m,wanamke huyo kuishi kwa shida pia kulazwa na mtoto alipougua na kulazwa katika kituo cha afya cha Tunduma na kuugunzwa na Daktari mkuu wa kituo hicho cha afya kwa gharama zake na hivi sasa anapatiwa hifadhi na Mwenyekiti wa Haki za binadamu Bwana Steven Ndege Ulaya.

Wakati huohuo wito umetolewa kwa wasamalia wema kuchangia chakula na ofisi za uhamiaji nchini ili kutumia mbinu ya kumrejesha nchini Kongo.

Juhudi za kumtafuta mwanaume huyo bado zinafanyika licha ya kumpata mjomba wake anayeitwa Abu mkazi wa Dar es salaam ambapo amekiri kumfahamu mwanamke huyo na kwamba na yeye anafanya juhudi za kumtafuta na kuwasiliana na uongozi wa kampuni ya KTM ili kuweza kunusuru afya ya mama na mtoto.

Jeshi la polisi mkoani Mbeya limethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger