Pages


Home » » JESHI LA POLISI LAWASHIKILIA WATU WATATU KWA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WAWILI - MBEYA

JESHI LA POLISI LAWASHIKILIA WATU WATATU KWA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WAWILI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 09:14 | 0 comments
Habari na mwandishi wetu.
Jeshi la polisi mkoani Mbeya watu watatu kwa kusababisha vifo vya watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi katika kijiji cha Ikuti wilayani Rungwe.

Marehemu wanakadiriwa kuwa na umri wa kuanzia miaka 25 - 30 ambao waliuawa kwa kupingwa na kundi la wananchi wenye hasira kali, baada ya kukamatwa kwa kosa la kuiba baada ya kuvunja duka mali ya Bwana Zkayo Ngela na kuiba bidhaa mbalimbali zenye thamani ya shilingi milioni 1,459,000.

Walikamatwa kuhusiana na tukio hilo kwa mahojiano zaini ni Bwana Andengulile George (47), Bwana Ernest Matola (49) na Bwana Moyo Mwasoni am,bao wote ni wakulima na wakazi wa Ikuti Kinyika wilayani humo.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Makandana Tukuyu na upelelezi zaidi wa tukio hili unaendelea.

Aidha majira ya saa 11:30 jioni eneo la Itewe barabara ya Mbeya/Iringa gari nambari T 471 BQA aina ya RAV 4 ikiendeshwa na dereva Gaston Kilembele (29), makazi wa Iyunga jijini Mbeya ilimgonga mtemea kwa miguu aitwaye Dora Mbinga (13)mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Mwashoma na kufariki dunia papohapo.

Dereva wa gari hiyo amekamatwa na gari limefikishwa kituo cha Polisi jijini Mbeya ambapo chanzo cha ajali hii kimetanjwa kuwa ni mwendokasi.

Wkati huohuo majira ya saa 2:15 usiku watu wasiofahamika eneo la Uyole jijini Mbeya walipora pikipiki nambari T 276 BRW aina ya T-BETTER iliyokuwa inaendeshwa na Vitus Mwenda (24) mkazi wa Airport jijini Mbeya.

Pikipiki hiyo yaenye thamani ya shilingi milioni 1,500,000 mali ya Bwana Gastus Liwa ilikodishwa na abiaria mmoja kutoka eneo la Kabwe jijini Mbeya kwenda eneo la Kilimo Uyole.

Mara baada ya kufika eneo la tukio dereva wa pikipiki alikuta watu wengine wawili ambao walimpora pikipiki hiyo. .

Kamnda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa matukio yote na kwamba upelelezi wa matukio haya unaendelea.

Zikiwa zimesalia siku mbili kumalizika kwa mwaka 2011 mkazi mmoja wa Ilemi aliyefahamika kwa jina la moja la Asifiwe (25 - 30) maarufu kama Tall amefukunzwa na wananchi katika mtaa wao baada kutuhumiwa kuchafua mazingira kwa kujisaidia ndani ya nyumba kisha kukituoa kinyesi chake katika mfereji wa maji unaopita kando kando ya nyumba anayoishi.

Tukio hilo limebainika majira ya saa mbili asubuhi watoto wakiwa wakicheza mpira na mpira kugongadirisha na kuingia ndani na walipoingia ndani kumfuata mwenyewe akiwa hayupo ndipo watoto hao wakagundua harufuya kinyesi chake ndani huku sehemu ya ukuta ikiwa imetobolewa usawa wa kiuno kwaajili ya kujisaidia haja ndogo.

Juhudi za kumpata Bwana ASifiwe ziligonga mwamba ukuta ndipo wananchi walipochukua jukumu la kuvitoa vyombo vyakenje na kumtaka ahame mara moja kwa kile ambacho wananchi wanadai kuwa anahatarisha afya za wakazi hao ambapo maji hayo huyatumia kwa shughuli mbalimbali.

Hata hivyo baadhi ya vyombo vyake zikiwemo sahani zimechomwa motona wananchi hao.

Wilayani Mbarali vijana wa timu ya Kata ya Utengule Usangu wameifunga Ofisi ya Mtendaji Joseph Kombora baada ya ofisi yake kushindwa kuwapatia usafiri wa gari kwenda kuhiriki mchezo wa mpaira wa miguu kugomea kikombe cha Mbunge wa Jimbo hilo Mwalimu Modestus Kilufi yanayoendeleakatika mji wa Rujewa.

Aidha Diwani wa Kata hiyo Bwana Juntwa Mwalyate amesema kata yake ni kubwa angeshirikishwa asingeshindwa kupata nauli hiyo imevunja moyo vijana wake, kwani Mtendaji alikuwa na nafasi ya kuwashirikisha Maafisa watendaji wote wa kaa hiyo.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger