Pages


Home » » WATOTO YATIMA WASAIDIWA WILAYANI CHUNYA - MBEYA

WATOTO YATIMA WASAIDIWA WILAYANI CHUNYA - MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:15 | 0 comments
 Waumini wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya wakipokea msaada hivi karibuni kutoka kwa Bi Sandra Witschi raia wa Uswisi, anayefanya kazi katika Jimbo hilo katika Idara ya Watoto na Wanawake.
 Bi Sandra Witschi akisisitiza watanzania kusaidia watoto yatima na kwamba watoto hao wakiendelezwa kielimu, nchi itaondokana na wimbi la ongezeko la watoto wa mitaani.
 Bi Sandra akiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima pamoja na walezi walioteuliwa kufuatilia maendeleo ya watoto hao kielimu, pamoja na maisha yao ndani ya jamii.
 Baadhi ya watoto 20 waliochaguliwa kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka huu wilayani Chunya, wakiwa katika picha ya pamoja na walezi wao baada ya kupokea msaada kutoka kwa Bi. Sandra Witschi hivi karibuni.(Picha na Ezekiel Kamanga, Chunya)

Hitimisho:- Bi Sandra Witschi ametoa msaada wa shilingi milioni 5.7 kwa watoto yatima wapatao 20, katika wilaya ya Chunya mkoani Mbeya kwa ajili ya kujiendeleza kielimu, fedha hizo zitatumika kwa ajili ya michango mashuleni, chakula pamoja na ada kwa mwaka mzima wa masomo.

Amesema kuwa zoezi hilo likifanyika kwa ufasaha litakuwa endelevu kwa watoto wengine na kisha ametoa ahadi ya kuwasomesha watoto hao mpaka kidato cha nne na wakifaulu wataendelea na masomo ya juu.

Bi Sandra ametaka jamii ya Kitanzania kuunga mkono mpango huo na kuwaimiza watoto yatima kupenda masomo yao na jamii kutowatumia kama watoto wa kazi za ndani.


Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger