Pages


Home » » KIKONGWE ABAKA - MBEYA

KIKONGWE ABAKA - MBEYA

Kamanga na Matukio | 07:05 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Kikongwe aitwaye Asagwile Kihaka (78) mkazi wa Kata ya Ghana jijini Mbeya, anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kubaka mwanafunzi wa darasa la saba (12) (jina lina limehifadhiwa), katika shule ya msingi Mbata jijini hapa.

Mtuhumiwa alitenda kosa hilo Desemba 14, mwaka uliopita nyumbani kwake baada ya kumrubuni mtoto huyo kwa kumtuma aende kununua kuni za shilingi 1,000 na kuagiza ampelekee nyumbani kwake, ndipo alipochukua jukumu la kumbaka mtoto huyo hadi kuzirai.

Binti huyo ambaye mpaka sasa hajaweza kusema kwa kinywa hadi jumapili ya Januari 8, mwaka huu ambapo alifanyiwa maombi katika kanisa la PHM lililopo jijini hapa, ambapo aliweza kuzungumzia tatizo hilo kwa maandishi na kudai kuwa mzee Kihaka ndiye aliyemtendea unyama huo.

Uchunguzi uliofanywa na Hospitali ya wazazi Meta umebaini kuwa binti huyo mara kadhaa amefikishwa hospitalini na kupatiwa matibabu ya homa, lakini hakuzungumza kilicho msibu hadi pale aliupokuja kuandika kuwa kabakwa na mzee huyo na kugundulika sehemu za siri zikiwa na michubuko na vidonda hali ambayo ilithibitishwa kuwa kaingiliwa na mwanaume.

Hata hivyo wananchi waliitisha mkutano wa hadhara kutokana na kuchoshwa na vitendo vya Mzee Kihaka ambapo imetajwa kuwa ni tukio la tatu la mzee huyo kutenda na viongozi wa Kata ya Ghana kumfumbia macho.

Mzee Kihaka alikamatwa Januari 2, mwaka huu na kupelekwa Kituo cha Polisi cha Kati cha Mkoa, ambapo Mtendaji wa Kata hiyo aliwasilisha barua ya kumwekea dhamana hali iliyopingwa na wakazi na kuamua kuitisha mkutano wa hadhara Januari 13 kwa hofu alikamatwa na kurudishwa mahabusu siku moja kabla ya mkutano huo wa hadhara Januari 12.

Wakati huohuo siku ya mkutano wa hadhara Diwani wa Kata hiyo Bwana Anjelo Chavaligino hakuhudhuria mkutano huo hali iliyopelekea kuleta hasira kwa wananchi hao na kisha kumtafuta hadi kumpata na kumleta kwenye mkutano huku akizomewa na wananchi wengine walienda kupiga mawe vioo vya nyumba ya Mzee Kihaka.

Mtandao huu umeshuhudia familia ya mzee huyo ikiangua kilio baada ya kunusurika na mawe hayo.

Jeshi la polisi mkoani Mbeya lilifika eneo la tukio na kuzuia ghasia hizo na Diwani wa kata hiyo Bwana Chavaligino ameahidi kuitisha mkutano ili kujadili mstakabali wa Mzee Kihaka, huku kwa upande wao wananchi wamemtaka Mzee huyo na familia yake kuhama eneo hilo.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger