Pages


Home » » WAFANYABIASHARA WA SOKO LA SOWETO JIJINI MBEYA WASITISHA MGOMO

WAFANYABIASHARA WA SOKO LA SOWETO JIJINI MBEYA WASITISHA MGOMO

Kamanga na Matukio | 05:11 | 0 comments
Taswira ya baadhi ya vibanda na bidhaa ya nyanya katika Soko la Soweto Jijini Mbeya.
*******
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Wafanyabiashara wa soko la Soweto Mbeya wamesitisha mgomo baada ya kuafikiana na halmashauri ya jiji la Mbeya kuhusu kupunguza ushuru wa biashara.

Mgomo wa wafanyabishara hao ulianza leo hii majira ya saa moja za asubuhi na ulidumu kwa muda wa masaa matatu, hata hivyo majira ya saa 4 za asubuhi wafanyabiashara hao waliendelea na biashara zao kama kawaida.

Wakiongea na mwandishi wetu baadhi ya wafanyabishara wa soko la Soweto walisema kupanda kwa kiwango cha ushuru kutoka shilingi mia mbili hadi mia tano, ni kikubwa na wao hawawezi kukabiliana nacho kutokana na kipato chao kuwa kidogo.

Kwa upande wake mkurugenzi wa jiji la Mbeya Juma Iddi alipoongea na mwandishi wetu kuhusu sakata hilo alisema kuwa mazungumzo kati ya uongozi wa Soko na Serikali yanaendelea vizuri na kwamba atatolea ufafanuzi mara baada ya kikao kumalizika.

Wakati huohuo tumepata taarifa kuwa madereva wa magari ya mizigo yafanyayo safari zake ndani na nje ya nchi wameanza mgomo wakidai kuwepo kwa usarasimu wa kuvuka mpaka wa Tanzania na Zambia katika upande wa Tanzania.
 
Naye Mkuu wa wilaya ya Mbeya Bwana Evans Balama amesema kuwa jiji linapaswa kukaa na wafanyabiashara hao ili kufikia muafaka, ili maamuzi yao yasiwaathiri wateja.
 
Hata hivyo mgomo huo wa wafanyabiashara umekuja mara baada ya Halmashauri ya jiji kupandisha ushuru kutoka shilingi 200 hadi shilingi 500, kwa wateja waliokuwa wakipanga bidhaa zao mezani na kwa vyumba kutoka shilingi 15,000 hadi kufikia 65,000 licha ya soko hilo awali kukosa wateja.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger