Pages


Home » » WAZIRI MAGHEMBE ZIARANI MBEYA AKUTANA NA WAKULIMA WA ZAO LA KAHAWA - MBOZI

WAZIRI MAGHEMBE ZIARANI MBEYA AKUTANA NA WAKULIMA WA ZAO LA KAHAWA - MBOZI

Kamanga na Matukio | 05:01 | 0 comments


 Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Profesa Jumanne Maghembe.
*****
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Profesa Jumanne Maghembe leo hii amekutana na wakulima wa zao la kahawa kutoka wilaya za Mbeya, Mbozi, Rungwe na Ileje kwa ajili ya kujadili mstakabali wa zao la kahawa.

Akiwa wilayani Mbozi, baadhi ya wakulima wa zao la Kahawa ambao walizuiwa kuhudhuria mkutano huo waliusimamisha msafara wa waziri Maghembe ikiwa ni ishara ya kushinikiza uongozi wa halmashauri kuwaruhusu kushiriki kwenye mkutano huo.


Baada ya tukio hilo mkuu wa mkoa wa Mbeya Bwana Abbas Kandoro aliwataka wakulima hao kuwachagua wawakilishi wao ambapo kila kikundi kiliwakilishwa na wajumbe wawili kushiriki katika mazungumzo hayo, lakini Mkuu wa mkoa huyo aliwataka wakulima kuteua wakulima kumi kuingia katika mkutano huo .

Katika mkutano huo baada ya kutokea mvutano mkubwa juu ya ununuzi wa kahawa mbivu na kavu Waziri Maghembe alikubaliana na uongozi wa mkoa wa Mbeya kwamba hawezi kutengua maamuzi yaliyoamuliwa ya kupiga marufuku ununuzi wa kahawa mbivu(cherry).
Awali wakulima wa zao la Kahawa wilayani Mbozi walikuwa wakiilalamikia Serikali kutoa upendeleo kwa makampuni yanayohusika na ununuzi wa kahawa na vikundi vinavyodaiwa kuwa ni vya vigogo ambavyo ndivyo vimetajwa kuhusika na urasimu licha ya mkulima kuendelea kuteseka kutokana na kukosa pembejeo za kisasa na hivyo kupata hasara kubwa ya kutunza kahawa.
Katika mjadala huo mwanasheria wa Wizara ya kilimo na ushirika alisema sheria inaruhusu kununua kahawa mbivu na ndio maana kikatolewa kibali kwa kampuni ya Lima kuendelea na ununuzi wa kahawa mbivu, ambapo kampuni hiyo ilikuwa ikiwasaidia wakuliwa kuwakopesha pembejeo. 

Wakati huohuo wakulima walishindwa kufahamu kilichoendelea kutokana na uongozi wa mkoa na wilaya kuwa wasemaje wakuu wa mkutano badala ya wakuliwa ili kutoa changamoto zao.

Aidha kuhusiana na Sakata la mwekezaji wa Kapunga Rice Project wilayani Mbarali Waziri Maghembe alipoulizwa na waandishi wa habari nje ya mkutano alishindwa kulitolea majibu na kudai kuwa atakuja kwa awamu nyingine ili kulizungumzia.

Alipoulizwa kuwa Je?, ana mkakati gani kuhusiana na wawekezaji kuua mifugo ya wafugaji na kufunga njia zote zianazoingia na kutoka shambani hapo, ambazo hutumiwa na wananchi katika shughuli zao za kiuchumi, Waziri Maghembe alisema haelewi chochote na wala hajapewa taarifa.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger