Meneja uzalishaji wa Kapunga Rice Project(KPR) Bwana Sergei Bekker(Kushoto), akitoa maelekezo kwa mwandishi wa habari Bwna Daniel Mbega kutoka gazeti la Mwananchi kuhusu ramani ya Mashamba ya Kapunga, alipotembelea shambani hapo..
******
******
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Mlinzi wa Shirika la Mpunga Kapunga Rice Project (KRP) wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya ameiba mali zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 10, baada ya kuvunja kufuri la kontena mali ya mwekezaji wa mradi huo.
Msemaji wa Kampuni hiyo aliyejitaja kwa jina moja Bwana Badri mwenye asili ya nchi ya Asia, amesema mali iliyoibiwa ni pamoja na madawa ya magugu, pampu na betri ambavyo vyote vina thamani ya dola elfu 7 za kimarekani, ambapo ni zaidi ya shilingi milioni 10 za kitanzania.
Bwana Badri amesema walishangaa kukuta silaha na risasi hizo zikiwa chini na mlinzi akiwa hayupo huku kontena likiwa tupu, mali ambazo waliziingiza katika kontena hilo siku chache zilizopita.
Hata hivyo tukio hilo halijaripotiwa Polisi hali ambayo imemshangaza Mkuu wa Polisi wilaya ya Mbarali, alipotembelea katika shirika hilo kwa masuala mengine.
0 comments:
Post a Comment