Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya Dokta Mary Mwanjelwa akizungumza na wananchi wa soko la sido Mwanjelwa jijini Mbeya, ataka watendaji wabovu kuondolewa ili kuweka heshima kwa serikali.
Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Mbeya Dk Mary Mwanjelwa akihutubia wananchi katikati ya madimbwi ya maji ya mvua huku akisisitiza kuwa ataenda kumwona mkurugenzi wa jiji la mbeya na kumwomba aje afukie madimbwi hayo huku wananchi wakimshangilia kwa ahadi hizo.
*****
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya Dokta Mary Mwanjelwa amehitimisha ziara yake ya siku nne katika jimbo la Mbeya Mjini, kwa kutembelea kata zote 36 na kuzungumza na wananchi. kupokea kero mbalimbali zinazowakabili pamoja na mchakato wa katiba.
Akizungumzia kero ya barabara jijini Mbeya linashughulikiwa kwa ukaribu kwani Mkandarasi ameshapatikana hivyo barabara ya kilometa 29 za kiwango cha lami zitajengwa, ili kuondoa adha wanazopata wananchi katika usafiri.
Hata hivyo amesisitiza wananchi mkoani Mbeya kuwasilisha kero zao kwake ili kuzifikisha kwa Idara husika, badala ya kukaa na kunung'unika ili waweze kupatiwa majibu sahihi.
Wakati huohuo amezitaka tofauti za kisiasa kuwekwa pembeni ili kuijenga Mbeya yenye mshikamano badala ya kusikia majanga yakiwemo moto na mafuriko ambayo yamerudisha nyuma maendeleo ya mkoa.
Dokta Mwanjelwa ameongeza kuwa amewataka viongozi kutimiza ahadi zao ili kuleta imani kwa wananchi.
0 comments:
Post a Comment