Basi la kampuni ya Mbarikiwe linalofanya safari zake kutoka Mkoa wa Mbeya kuelekea Sumbawanga limepinduka jana, majira ya saa 1 asubuhi, katika mteremko wa milima Mbalizi, na kusababisha abiria zaidi ya 40 kujeruhiwa.
Pichani baadhi ya wananchi waliofika eneo la tukio wakiliinua Basi la kampuni ya Mbarikiwe linalosafirisha abiria kutoka Mkoa wa Mbeya kuelekea Sumbawanga baada ya kupinduka jana, majira ya saa 1 asubuhi, katika mteremko wa milima Mbalizi, na kusababisha abiria zaidi ya 40 kujeruhiwa.
Uinuaji wa basi la Mbarikiwe ulisababisha kusimama kwa shughuli za usafirishaji kwa takribani dakika 15.
******
Habari na Picha na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Basi la kampuni ya Mbarikiwe linalofanya safari zake kutoka Mkoa wa Mbeya kuelekea Sumbawanga limepinduka jana katika mteremko wa milima Mbalizi, na kusababisha abiria zaidi ya 40 kujeruhiwa.
Tukio hili limetokea jana majira ya saa moja asubuhi ambapo basi hilo ambalo nambari za usajili liling'olewa na mmiliki ili kuficha ukweli wa ajali hiyo na kisha ondolewa pasipo kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi mkoani hapa, kupewa ruhusa ya gari kuondolewa au kutolewa nambari za usajili.
Hata hivyo baada ya taarifa ya ajali hiyo kutolewa kwa Jeshi la Polisi hawakuweza kufika eneo la tukio hadi pale basi hilo lilivyoondolewa eneo la tukio.
Aidha basi hilo ni moja ya magari mabovu yanayosafirisha abiria mkoani Mbeya huku jeshi la Polisi likifumbia macho, licha ya Serikali kutangaza mabasi yaliyobadilishwa katika mfumo wa roli kuacha kusafirisha abiria.
Kwa upande wake mmoja wa abiria walionusurika katika ajali hiyo amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi na kuharibika kwa mfumo wa breki hali iliyopelekea dereva wa basi hilo kushindwa kumudu na kisha kupinduka upande wa kushoto mwa barabara ya Mbeya/Tunduma na majeruhi wote walikimbizwa katika hospitali ya Rufaa na Ifisi mkoani Mbeya.
0 comments:
Post a Comment