Pages


Home » » WANANCHI WA KATA YA GHANA WAMTAKA MBAKAJI MZEE KIHAKA KUHAMA MAKAZI - MBEYA

WANANCHI WA KATA YA GHANA WAMTAKA MBAKAJI MZEE KIHAKA KUHAMA MAKAZI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 06:37 | 0 comments
Baada ya kuitishwa kwa mkutano wa kujadili sakata la Mzee Asangile Kihaka (78) kumbaka binti wa miaka 12, mwanafunzi wa darasa la 7 katika Shule ya Msingi Mbata. Mkutano huo ulifanyika katika Ofisi za Kata ya Ghana na kuhudhuriwa na viongozi wa kata, Jeshi la polisi na wananchi wa kata hiyo. Pichani ni mmoja wa majirani akiwa ameshika bahasha na kusalimiana na baadhi ya viongozi, baada ya diwani wa kata hiyo Bwana Angelo Chavaligino kutoa pole kwa baba mzazi wa mtoto aliyebakwa Bwana Ekson Nazareth (47), ambaye pia ni mzee wa baraza mahakama ya Mwanzo ya Mbeya Mjini.
Afande L.M.Kiyeyeu wa Jeshi la polisi mkoani Mbeya kutoka kitengo cha Polisi na ulinzi shirikishi akitoa elimu ya ulinzi shirikishi kwa wananchi wa Kata ya Ghana jijini Mbeya lakini alikuwa katika wakati mgumu, wananchi wakipinga vikali rushwa na sheria iliyotumika kumpa dhamana na kuchelewa kufikishwa mahakamani Mzee Asangile Kihaka (78) kwa tuhuma za kumbaka binti wa miaka 12, mwanafunzi wa darasa la 7 katika Shule ya Msingi Mbata, ambapo ni tukio la tatu la mzee huyo kutenda.
  Diwani wa Kata ya Ghana Bwana Angelo Chavaligino akitoa utetezi wake baada ya kushindwa kufika kwa wakati muafaka katika mutano wa awali wa kumjadili Mzee Asangile Kihaka (78) mpaka pale alipofuatwa katika mkutano wa kabila la Wahehe  uliofanyika Januari 13, mwaka huu eneo CCM kata ya Ghana, alikokuwa amehudhuria.
 Mmoja wa wananchi wa eneo la Ghana akilaani vikali kitendo cha Mzee Asangile Kihaka (78) kumbaka binti wa miaka 12, mwanafunzi wa darasa la 7 katika Shule ya Msingi Mbata, ambapo ni tukio la tatu la mzee huyo kutenda.
 Diwani wa Kata ya Ghana Bwana Angelo Chavaligino na Mwenyekiti wa mkutano huo Bwana Kyejo (walioshikana mikono), kabla ya kuanza kwa mkutano wa kujadili sakata la Mzee Asangile Kihaka (78) kumbaka binti wa miaka 12, mwanafunzi wa darasa la 7 katika Shule ya Msingi Mbata, ambapo ni tukio la tatu la mzee huyo kutenda..
 Mmoja kati ya askari mstaafu wa Jeshi la polisi anayeishi mtaa huo ambaye pia akilaani vikali kitendo cha Mzee Asangile Kihaka (78) kumbaka binti wa miaka 12, mwanafunzi wa darasa la 7 katika Shule ya Msingi Mbata, ambapo ni tukio la tatu la mzee huyo kutenda.
 Baba mzazi wa binti aliyebakwa Bwana Ekson Nazareth  (47), ambaye pia ni mzee wa baraza mahakama ya Mwanzo ya Mbeya Mjini.. Hata hivyo mzazi huyu wa binti aligoma kabisa kusogea kwenye mkutano huo cha wakazi wa ghana.(Picha na Ezekiel Kamanga na Mbeya Yetu).

Hitimisho:- Mkutano ulimalizika kwa amani na kuazimia Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Bwana Evans Balama kukubali ombi la wananchi wa kata ya Ghana kumtaka Mzee Asangile Kihaka kuhama katika makazi yake na kwamba hafai katika jamii kutokana na vitendo vyake vya ubakaji.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger