Pages


Home » » JINAMIZI LA MAUAJI LAZIDI KUITEKETEZA MBEYA, WANNE WAFARIKI KWA MATUKIO TOFAUTI

JINAMIZI LA MAUAJI LAZIDI KUITEKETEZA MBEYA, WANNE WAFARIKI KWA MATUKIO TOFAUTI

Kamanga na Matukio | 01:05 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Watu wanne  wamefariki dunia mkoani Mbeya katika matukio manne tofauti yaliyotokea mwishoni mwa juma.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa Advocate Nyombi amesema tukio la kwanza limetokea majira ya saa tatu usiku eneo la Ilemi jijini Mbeya, mtu mmoja aitwaye Ibrahimu Mwakyoma (41), ambaye ni fundi cherehani alijeruhiwa kwa kupingwa na kitu kizito kichwani na mtu au watu wasiofahamika.


Marehemu alivamiwa wakati akitokea katika shughuli zake na chanzo cha tukio hili hakijafahamika, ambapo baada ya kutendewa ukatili huo Bwana Mwakyoma aliokotwa na wananchi na kupelekwa katika hospitali ya rufaa jijini Mbeya ambapo alifariki dunia wakati anapatiwa matibabu na kisha mwili wake kuhifadhiwa hospitalini hapo huku msako mkali ukiendelea ili kuweza kuwabaini waliohusika na tukio hilo.


Aidha majira ya saa 5:15 usiku huko kijiji cha Biti Manyanga wilaya ya Chunya Paulo Leonard (20) ambaye ni mkulima alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Zahanati ya Kijiji hicho baada ya kupingwa na kitu butu na Salum Rashid.


Chanzo cha mauaji hayo ni tuhuma za wizi baada ya marehemu kuiba miche ya Tumbaku kwenye kitalu cha mtuhumiwa.


Mtuhumiwa alitoroka mara baada ya tukio na upelelezi wa tukio hili unaendelea.


Wakati huohuo majira ya saa 10:30 jioni katika kijiji cha Miembeni wilaya ya Chunya gari nambari T 311 ADS Toyota Staut iliyokuwa ikiendeshwa  na dereva aitwaye Boko Katingu (30) ilimgonga mpanda pikipiki aitwaye Hansi Katete (46), ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Saza wakati akiendesha pikipiki yenye namba T  427 BRF na kufariki dunia muda mfupi akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Mwambani.


Bwaba Hansi alimbeba abiria mmoja katika pikipiki yake aitwaye Maligumu Meza (80) mkazi wa Saza ambaye amevunjika mguu mmoja na kulazwa katika hospitali ya Mwambani.


Chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi na dereva wa gari amekimbia na gari yake kufikishwa katika Kituo cha Polisi.


Tukio lingine Mtu mmoja amefariki dunia baada ya wananchi kumtuhumu kuiba karanga wilayani Mbozi ambapo majira ya saa 2:27 katika kitongoji cha Hatelele wilaya ya Mbozi ambapo wananchi wenye hasira kali walimkamata mtuhumiwa kwa madai ya kuiba karanga ambazo alizipakia katika baiskeli yake.


Kwa mujibu ya wananchi hayo karanga hizo ni sehemu ya debe tisa zilizoibiwa mali ya Fengo ambaye ni mkazi wa kijiji hicho aliyedai kuibiwa.


Baada ya kipigo wananchi hao waliochoma moto mwili wa marehemu ambapo uliteketea kabisa.


Kwa upande wake Mtendaji wa Kijiji cha Hatelele Bwana Petro alitoa taarifa za tukio hilo kwa mwenyekiti wa kijiji Bwana Simon Kibona ambaye alitoa taarifa kwa kituocha cha Polisi cha Mlowo , ambapo walifika eneo la tukio na kuamuru mwili wa marehemu kuzikwa paho hapo pembeni ya mto Mlowokutokana na mwili huo kuharibika vibaya.


Marehemu anakadiliwa kuwa na umri wa miaka 26 na inadaiwa kuwa alikuwa ni mkazi wa kijijicha Msia wilayani humo na baiskeli yake imehifadhiwa katika Kituo cha Polisi Mlowo na hakuna aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

 Kamanda wa Polisi mkoani hapa Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa matukio yote na jeshi lake linafanya uchunguzi ili kubaini watu waliohusika na matukio yote.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger