Pages


Home » » MAWAZIRI KUWENI MAKINI MNAPOPOKEA TAARIFA ZA MAENDELEO MIKOANI.

MAWAZIRI KUWENI MAKINI MNAPOPOKEA TAARIFA ZA MAENDELEO MIKOANI.

Kamanga na Matukio | 07:10 | 0 comments
Waziri wa Chakula, Kilimo na Ushirika Profesa Jumanne Maghembe.
Diwani wa Kata ya Halungu, Wilayani Mbozi Samson Simkoko akizungumza na wakulima wa kata hiyo katika mkutano kuhusiana na ukwasi wa pembejeo za kilimo kutokana na baadhi ya makampuni  ya kusambaza Mbolea kusitishwa wilayani humo kwa kile kilichodaiwa makampuni hayo kuwanyonya wakulima hali ambayo imedaiwa kuwa si kweli kwa manufaa ya wachache.
 Baadhi ya wakulima waliohudhuria mkutano wa kujadili ukwasi wa pembejeo za kilimo kutokana na baadhi ya makampuni  ya kusambaza Mbolea kusitishwa wilayani humo kwa kile kilichodaiwa makampuni hayo kuwanyonya wakulima hali ambayo imedaiwa kuwa si kweli kwa manufaa ya wachache.
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Halungu Bwana Charles Simkoko ambaye alikuwa mwenyekiti wa Mkutano wa Ukwasi wa pembejeo za kilimo kutokana na baadhi ya makampuni  ya kusambaza Mbolea kusitishwa wilayani humo kwa kile kilichodaiwa makampuni hayo kuwanyonya wakulima hali ambayo imedaiwa kuwa si kweli kwa manufaa ya wachache.
 Pichani juu ya nyumba ni Solar ambayo ililetwa kwa matumizi ya kuandikisha hati za kimila ambayo ilifunguliwa na mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dk Jakaya Kikwete lakini hali ni tofauti baada ya kompyuta kuchukuliwa na wakubwa Wilayani na kisha kurejeshwa bila Printer na hivyo kusisimama kwa zoezi hilo.
*****
Habari na Chanzo chetu.
Mawaziri wa Serikali ya Tanzania wametakiwa kufika vijijini na kuzungumza na wananachi ili kuwianisha takwimu za maendeleo wanazopewa na Wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya ambapo takwimu nyingi zinakuwa ni za kupika na maamuzi ni yale ya matakwa ya baadhi ya vigogo pasipokushirikishwa wananchi.

Hayo yameelezwa na diwani ya kata ya Halungu iliyopo wilayani Mbozi mkoani Mbeya Samson Simkoko alipokuwa akizungumza na wakulima wa kahawa wa kata hiyo leo ambao wote wamekosa pembejeo na kuamua kuomba katika kampuni ya Lima na makampuni mengine binafsi yawasaidie mbolea.

Uchunguzi uliofanywa na kikosi kazi cha mtandao huu, umebaini kuwa tarere 17 mwaka huu 2012 Waziri wa kilimo na chakula Prof, Jumanne Maghembe atasomewa taarifa inayokinzana na wananchi hasa katika wilaya ya Mbozi kunakotarajiwa kuibuka mzozo wa maslahi ya zao la kahawa.

Hata hivyo hayo yamekuja baada ya mtandao huu kufichua siri ya hatua ya baadhi ya viongozi wa wilaya mkoani Mbeya wanaotuhumiwa kumdanganya mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, katika masuala ya uchumi.

Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa mkakati huo umejikita katika nyanja mbili za kiuchumi na kisiasa ambapo wilaya za Mbozi na Rungwe zimetajwa kuwa vinara wa mkakati huo.

Hadidu za rejea za kikao kimoja cha wadau wa kahawa mkoa wa Mbeya kilichofanyika katika ukumbi wa Mkapa na kusimamiwa na mkuu wa wilaya ya Mbozi, Gabriel Kimolo, Septemba 15,2011 ni Dondoo Na.5 juu ya ununuzi wa kahawa mbichi (Red Cherry).

Katika kipengele hicho mkuu wa mkoa ameelezwa kuwa kilimo cha kahawa hakimnufaishi mkulima wa zao hilo la biashara hasa anapouza kahawa ya matunda na kwamba mkulima akiuza kahawa hiyo anapata hasara ukilinganisha na kuuza kahawa kavu (parchment coffee).

‘Kilo tano za kahawa mbichi hutoa kilo moja ya kahawa kavu, kahawa mbichi inapouzwa shilingi 200 kwa kilo, kahawa kavu inauzwa kwa shilingi 3,500 hadi 5,000 kwa kilo,’’ unabainisha muhtasari wa kikao hicho jambo ambalo si la kweli.

Uchunguzi umebaini kuwa kahawa mbichi inanunuliwa kwa bei tofauti tofauti ambapo makampuni yanayolipa kodi hununua kahawa hiyo kwa shilingi 1,000 mpaka 1,200 na vikundi hununua kahawa hiyo mbichi kwa shilingi 600-800.

Mbali na suala hilo ambalo mizizi yake iko katika wilaya ya Mbozi kunakoelezwa kuwa baadhi ya watumishi wanafaidika na biashara hiyo, mkuu wa mkoa wa Mbeya hivi karibuni amepokea barua ya kuanza kumwonyesha dira ya watendaji wa wilaya ya Rungwe ambao pia wanahusishwa katika mikakati hiyo ya kumdanganya mkuu huyo wa mkoa.

Barua hiyo kutoka katika kampuni mojawapo inayonunua kahawa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini imemweleza Kandoro jinsi kampuni hiyo ilivyoporwa mamilioni ya fedha na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Rungwe

Barua hiyo ya Oktoba 20 mwaka 2011ambayo mtandao huu wa www.kalulunga imepata nakala yake, katika kipengele cha 6 imeweka bayana kuwa Julai 11,2011, Halmashauri ya Rungwe ilipora kahawa mbichi kilo 462, Julai 14,2011, kilo 1,090 na Julai 18,2011 ilipora kilo 21 pamoja na mizani kisha kahawa hiyo kuiuza na Oktoba 13,2011.

Ilijaribu tena kupora kilo 8,100 ambazo baada ya uongozi wa kampuni hiyo kujitokeza na kulalamikia uporaji huo halmashauri hiyo akaamua kuiachilia kahawa hiyo.

Hivyo barua hiyo imemuomba mkuu huyo wa mkoa wa Mbeya kuangalia lalamiko lao na kulitafutia ufumbuzi ambapo nakala ya barua hiyo yenye kurasa tatu imepelekwa nakala zake kwa Katibu wa Waziri Mkuu, Ikulu, Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Katibu Muu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, mkuu wa wilaya ya Rungwe, mwenyekiti wa TCBA na mkurugenzi mkuu Mamlaka ya Kahawa Tanzania.

Baadhi ya makampuni yanayonunua mazao ya biashara mkoani Mbeya ni Biooland, Mavuno, Lima. Unyiha na Oran.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger