Mtoto Oscar Oliver (17), mkazi wa Ilemi darajani Jijini Mbeya akiwa nyumbani kwa Mjomba wake Bwana Andendekisye Mwakagugu aliyekanusha kumchoma moto mtoto huyo na kudai kuwa wakati akimuadhibu baada ya kumkuta akitaka kuiba sehemu ya biashara, ndipo alipoangua katika jiko la moto lililokuwa karibu licha ya Jeshi la Polisi kumshinikiza mtoto huyo aseme ameunguzwa na moto.
Mjomba wake alikamatwa na kupewa kipigo kikali na watuhumiwa ambao waliamriwa kumuadhibu bila sababu za msingi wakati wote niwatuhumiwa.
Uchunguzi zaidi umebaini kuwa mtoto huyo ni mtukutu wa muda mrefu ambapo amewahi kufukuzwa wilayani Rungwe kwa tuhuma za wizi na pia miezi miwili iliyopita ametoka kutumikia kifungo cha miezi miwili baada ya kuhukumiwa kutenda kosa la wizi katika duka la madawa eneo la Nzovwe jijini Mbeya, ambapo aliiba bidhaa na pesa shilingi milioni 9 na kuhukumiwa katika Mahakama ya Mwanzo jijini hapa.
Mwandishi wa habari hii ameshuhudia mtoto huyo akiomba msamaha mbele ya mjomba wake kuwa hatojihusisha tena na vitendo vya wizi, ambapo mjomba wake ameendelea kuuguza vidonda vya mtoto huyo na kuripoti Kituo cha Polisi cha Kati mara kwa mara.
Hata hivyo Mwenyekiti wa mtaa huo Bwana Mwakibete amekiri kupokea kwa malalamiko ya wizi uliokithiri wa mtoto huyo. (Picha na Ezekiel Richard Kamanga)
0 comments:
Post a Comment