Pages


Home » » UNYANYAAJI WA KIJINSIA:- MWANAMKE APIGWA , AFUNGIWA SIKU TATU NDANI BILA KUPEWA MATIBABU - MBEYA

UNYANYAAJI WA KIJINSIA:- MWANAMKE APIGWA , AFUNGIWA SIKU TATU NDANI BILA KUPEWA MATIBABU - MBEYA

Kamanga na Matukio | 04:49 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Bi Judith Mnyape (32) mkazi wa Ghana Magharibi jijini Mbeya amepingwa na mumewe Bwana Clemence Luhimbo (36), maarufu kwa jina la Kidevuna kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kile kilichodaiwa na kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Tukio hilo limetokea Januari 14, mwaka huu majira ya saa 2 usiku nyumbani kwake ambapo mume alimpiga mkewe kwa kwa kutumia ufagio hadi kuvunjika hali iliyompelekea mwanamke huyo kupata majeraha na kisha kulazwa katika hospitali ya Rufaa jijini Mbeya Januari 20 hadi 21 mwaka huu.

Mbali ya kumpiga mkewe Bwana Luhimbo, maarufu kwa jina la Kidevu ambaye ni dereva wa taksi anayeegesha kituo cha Baa ya Kalembo iliyopo Sokomatola, alimfungia mkewe kwa muda wa siku tatu fululizo pasipo kupewa huduma yoyote ya matibabu.

Uchunguzi wa mtandao huu umebaini kuwa mbali na kumfungia vile vile Bwana Luhimbo anadaiwa kumwingiza chupa ya soda kwa siku tatu mfululizo  mkewe sehemu za siri kwa madai kuwa amechoshwa na vitendo vya ukahaba vinavyofanywa na mkewe.

Bwana Luhimbo anahojiwa na Kituo cha Polisi cha Kati, kitengo cha kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto ambapo mpaka sasa wamemtaka kuhakikisha mkewe anapatiwa matibabu ipasavyo, huku akiendelea kuripoti polisi.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger