Pages


Home » » UPUNGUFU WA MADAWATI WASABABISHA WANAFUNZI KUKAA CHINI NA WENGINE WANNE KATIKA DAWATI MOJA - MBEYA

UPUNGUFU WA MADAWATI WASABABISHA WANAFUNZI KUKAA CHINI NA WENGINE WANNE KATIKA DAWATI MOJA - MBEYA

Kamanga na Matukio | 07:02 | 0 comments
Wanafunzi wa Shule ya msingi Mbata Kata ya Ghana jijini Mbeya, wanaketi chini na wengine kulazimika kukaa wanafunzi wanne bala ya ya watatu katika dawati moja kutokana shule hiyo kukabiliwa na upungufu wa madawati.
 Baadhi ya wanafunzi ambao walionekana wakiwa wamechuchumaa au kuketi chini.
*****
Habari na Picha na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Wanafunzi wa Shule ya msingi Mbata Kata ya Ghana jijini Mbeya, wanaketi chini kutokana shule hiyo kukabiliwa na upungufu wa madawati.

Hayo yamebainishwa na mtandao huu walipotembelea shuleni hapo na kukuta wanafunzi zaidi ya 20 wa darasa la sita wakiwa wamechuchumaa kwakukosa madawati na wengine kukaa katika dawati wanafunzi wanne badala ya watatu.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Bi Betty Mwakalinga amesema jukumu la kutatua tatizo la madawati lipo juu yake kwani ni jukumu la Kamati ya shule inayoongonzwa na Mwenyekiti Bwana Philemon Mwansasu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya Shule Bwana Philemon amesema kuwa shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 900 na wanajumla ya madawati mazima 150 na wanaupungufu wa madawati 325, ambapo walikubalina na wazazi katika kikao kilichofanyika mwezi Novemba mwaka uliopita na kukubaliana kila mzazi kuchanga shilingi 10,000 kwa kila mwanafunzi kuanzia darasa la pili hadi la saba na shilingi 15,000 kwa mwanafunzi wa darasa la kwanza.

Ameongeza kuwa kila dawati lina gharimu shilingi 40,000/= ambapo watoto wanne wangemudu kununua dawati moja, lakini kumekuwa na mvutano baina ya diwani wa Kata hiyo Bwana Anjelo Chivaligano (CCM)  na Kamati ya Shuleni, kutokana na diwani huyo kumtaka kila mwanafunzi kuchangia shilingi elfu mbili, na kwamba wanafunzi 20 wanamudu kununua dawati moja na hivyo kuleta ukwasi kutokana na kushindwa kumudu na kutatua tatizo la upungufu wa madawati

Hata hivyo mwaka 2010 Serikali ilitoa madawati 10 kwa shule hiyo na kwa sasa inatoa ruzuku ya elfu 90 kila baada ya miezi mitatu kwa shule hiyo na kwamba hali hiyo itakuwa ni ndoto kumudu gharama za ueneshaji wa taaluma shuleni hapo .

Wakati huohuo shule hiyo inaupungufu wa vyoo kutokana na kuwa na matundu 14 na kukosa maji, ambapo mtandao huu umeshuhudia kuwepo kwa foleni.

Serikali hivi karibuni ilipinga utolewaji wa michango mashuleni huku ikishindwa kutolea njia mbadala zauendeshaji wa shule hizo na mambo ya kisiasa kuchangia kudhorota kwa maendeleo katika Kata mbalimbali jijini Mbeya.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger