Pages


Home » » KABURI LAFUKULIWA BAADA YA POLISI KURUHUSU KUZIKA KWA TUHUMA ZA WIZI.

KABURI LAFUKULIWA BAADA YA POLISI KURUHUSU KUZIKA KWA TUHUMA ZA WIZI.

Kamanga na Matukio | 05:38 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbozi.
Jeshi la polisi mkoani Mbeya limeingia lawamani baada ya wananchi mbalimbali kulalamikia utendaji kazi wa Jeshi hilo baada ya kukumbatia vitendo vya kihalifu vinavyofanywa wilaya ya Mbozi, mkoani Mbeya, kutokana na kukinzana na dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi.

Mnamo Januari 15, mwaka huu siku ya Jumapili, Jeshi la polisi kutoka Kituo cha Mlowo wilayani Mbozi walilazimishwa kufukua kaburi la kijana mkazi wa Msiha aliyeuawa hivi karibuni kwa tuhuma za wizi wa debe moja la karanga mali ya Sengo, katika kitongoji cha Nyelya, kijiji cha Hatelele na kisha kuchomwa moto na kuzikwa bila ndugu zake kufahamu, huku jeshi hilo likishindwa kuwakamata waliohusika na mauaji hayo.

Baada ya ndugu wa marehemu kupata taarifa za ndugu yao kuuawa walikwenda mahakamani kupata kibali cha kufukua mwili huo ambao ulifukuliwa majira ya saa 7 mchana na kwenda kuzikwa katika kijiji cha Msiha.

Kituo cha Mlowo ni moja ya kituo kinacholalamikiwa na kwa kusababisha mauaji kwa watu wanaouhumiwa kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya wizi, ambapo Mkuu wa kituo hicho kuagizwa kuwa mhalifu afikishe kituoani hapo akiwa ameuawa na sio hai.

Hayo yamethibitishwa na Mwenyekiti wa haki za Binadamu wa wilaya hiyo Bwana Bruno Mwambene na kuthibitishwa na mwenyekiti wa mkoa Bwana Said Madudu ambapo walionesha nyaraka mbalimbali za malalamiko ya wananchi ambao ni ndugu wa watu waliouawa.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger