Mfugaji Bwana Mungo Makubi (27) kushoto na Singu Mwakami (23) wakimtazama ng'ombe aliyeuawa kwa kugongwa na gari aina ya Toyota Landcruiser lenye nambari ya usajili T 566 BQH. iliyokuwa ikiendeshwa na mwekezaji wa Kapunga Rice Project wilayani Mbarali aitwaye Bwana Gerry Baquzein baada ya kuwakosa wafugaji hao baada ya kujistiri nyuma ya mti na kisha hasira za mwekezaji kuishia kwa kumgonga ng'ombe huyo mwenye thamani ya shilingi laki 6 za kitanzania na kisha kufa papo hapo.
Gari aina ya Toyota Landcruiser lenye nambari ya usajili T 566 BQH. iliyokuwa ikiendeshwa na mwekezaji wa Kapunga Rice Project wilayani Mbarali aitwaye Bwana Gerry Baquzein na kisha kumgonga ng'ombe mwenye thamani ya laki 6 na kisha kufa papo hapo, baada ya kuwakosa wafugaji hao baada ya kujistiri nyuma mti.
Jeshi la polisi lilifika eneo la tukio na kushuhudia ng'ombe huyo akiwa amefariki lakini hawakuchukua hatua zozote za kisheria dhidi ya mwekezaji wa Kapunga Rice Project wilayani Mbarali aitwaye Bwana Gerry Baquzein, aliyetumia gari lake kufanya mauaji ya ng'ombe huyo.
Wafugaji wakionesha jinsi mwekezaji huyo alivyokuwa akiwakimbiza na pichani ni alama za magurudumu ya gari yalipopita wakati akiwafukuza.
Sehemu ya shamba ambayo mwekezaji wa Kapunga Rice Project ameshindwa kuilima na nyasi zikiendelea kuota.
Moja ya mitambo inayotumika katika shughuli katika shamba hilo la Kapunga Rice Project ikiwa imeachwa katika moja ya sehemu ya shamba ambayo mwekezaji ameshindwa kuilima, na nyasi kuendelea kuota.
Baada ya mwekezaji wa Kapunga Rice Project kufunga njia zinazoingia na kutoka, pia kufunga maji ya bomba wananchi wa kijiji cha Kapunga wapo katika hatari kubwa kama inavyooneka pichani, wanawake wakivuka kuelekea ng'ambo ya pili kwa kutumia gogo.
Baadhi ya akina mama wakiteka maji baada ya mwekezaji kufunga maji ya bomba, hali ambayo inatishia kuhatarisha afya zao kutokana na maji hayo kutumika kufulia nguo, kuoga na kunywesha mifugo ndani ya mtu huo.(Picha na Ezekiel Kamanga, Mbeya)
0 comments:
Post a Comment