UFAFANUZI:- Ukarabati wa barabara wa aina yake tofauti na utaalamu yakinifu, Mkurugenzi wa Jiji Bwana Juma Idd amesema hatua hii ni ya muda kwani barabara hiyo imetengewa jumla ya shilingi milioni 400, ambapo Mkandarasi amekwisha patikana na shughuli za ukarabati zitaanza mara baada ya msimu wa mvua kuisha.
Mtandao huu umeshuhudia ukarabati ukiendelea eneo la Kanisa la Sabato barabara ya Mbalizi kutokea Meta jijini hapa ambapo Saruji imetumika kuziba viraka katika barabara hiyo, badala ya kutumia Lami ambapo huigharimu serikali kutokana na viraka hivyo kubanduka baada ya muda mfupi.
Hata hivyo mwaka uliopita barabara hiyo iligharimu shilingi milioni 57, licha ya Mkurugenzi huyo kutokuwa tarai kutaja kiasi cha gharama zilizotumika kukarabati barabara hiyo kwa mwaka huu na kudai kuwa ni kiasi kidogo kimetumika.
Wakati huo huo Baraza la madiwani wa Kata zote 36 za jiji la Mbeya limelalamika kuwepo kwa miundombinu mibovu ya barabara hizo na utendaji mbovu wa makandarasi ambao huzijenga barabara hizo licha ya kupewa pesa nyingi.
0 comments:
Post a Comment