Pages


MTOTO AFUNGWA KAMBA YA KATANI MIGUU NA MAMA YAKE

Kamanga na Matukio | 05:15 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Bi Rahabu Robert (26) mkazi wa mtaa wa Manga A, jijini Mbeya amekutwa amemfunga kamba ya katani kwenye meza mtoto wake wa kumzaa aitwaye Eliza Frank (4), kwa kile alichodai kuchoshwa na tabia mbaya ya uzurulaji.

Tukio hilo limetokea Januari 25, mwaka huu nyumbani hapo majira ya saa 10 jioni na mtoto huyo kukutwa majira ya saa 12 jioni na majirani wakati mama huyo akiwa kanisani kwenye ibada.

Baada ya majirani kubaini ukatili huo walimtaarifu Mwenyekiti wa mtaa Bi Rose Mwaisanga, ambapo naye alimfuata mama huyo kanisani katika Kanisa la Moravian Ruanda lililopo karibu na Hospitali ya K'S lililopo mtaa wa Mafiati.

Wakati huo huo baada ya kufika nyumbani mama huyo na mwenyekiti walimkuta mtoto huyo akilia kwa uchungu kutokana na maumivu makali ya kamba hiyo, na kulazimika kumfungua mtoto na mama wa mtoto huyo kufikishwa katika Kituo cha Polisi cha Kati.

Mwenyekiti wa mtaa huo Bi Rose na mwandishi wa mtandao huu walikuwa na wakati mgumu wa kumnusuru mama huyu asipigwe na wananchi wenye hasira kali, kutokana na kumpiga mama huyo pasipo kujali mtoto mchanga aliyembeba mgongoni na kuingizwa kwenye daladala hali ambayo ilisababisha wananchi hao kuipiga mawe daladala hiyo wakidai mama huyo naye aadhibiwe.

Kwa upande wake Baba mzazi wa mtoto huyo Bwana Frank Anangisye (29), amesema kuwa alikuwa hana taarifa yoyote juu ya mateso ya mwanae na kuwashukuru majirani kwa kuweza kufichua uovu wa mkewe.

Hata hivyo mama wa mtoto huyo Bi Rahabu anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote baada ya uchunguzi wa Jeshi la polisi kukamilika. 

UNYANYAAJI WA KIJINSIA:- MWANAMKE APIGWA , AFUNGIWA SIKU TATU NDANI BILA KUPEWA MATIBABU - MBEYA

Kamanga na Matukio | 04:49 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Bi Judith Mnyape (32) mkazi wa Ghana Magharibi jijini Mbeya amepingwa na mumewe Bwana Clemence Luhimbo (36), maarufu kwa jina la Kidevuna kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kile kilichodaiwa na kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Tukio hilo limetokea Januari 14, mwaka huu majira ya saa 2 usiku nyumbani kwake ambapo mume alimpiga mkewe kwa kwa kutumia ufagio hadi kuvunjika hali iliyompelekea mwanamke huyo kupata majeraha na kisha kulazwa katika hospitali ya Rufaa jijini Mbeya Januari 20 hadi 21 mwaka huu.

Mbali ya kumpiga mkewe Bwana Luhimbo, maarufu kwa jina la Kidevu ambaye ni dereva wa taksi anayeegesha kituo cha Baa ya Kalembo iliyopo Sokomatola, alimfungia mkewe kwa muda wa siku tatu fululizo pasipo kupewa huduma yoyote ya matibabu.

Uchunguzi wa mtandao huu umebaini kuwa mbali na kumfungia vile vile Bwana Luhimbo anadaiwa kumwingiza chupa ya soda kwa siku tatu mfululizo  mkewe sehemu za siri kwa madai kuwa amechoshwa na vitendo vya ukahaba vinavyofanywa na mkewe.

Bwana Luhimbo anahojiwa na Kituo cha Polisi cha Kati, kitengo cha kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto ambapo mpaka sasa wamemtaka kuhakikisha mkewe anapatiwa matibabu ipasavyo, huku akiendelea kuripoti polisi.

MWANAMKE APANDISHWA KIZIMBANI KWA KOSA LA KUMUUA MWANAE - MBEYA

Kamanga na Matukio | 04:27 | 0 comments

Habari na Mwandishi wetu
Neema Edson mwenye umri wa miaka 19 mkazi wa Namtanga Swaya jijini Mbeya amefikishwa katika mahakama ya mkoa kwa kosa la kumuua mtoto wake akiwa mchanga.

Akisoma shitaka hilo mbele ya hakimu mkazi mfawizi Monika Ndyekobola mwanasheria wa serikari Ema Msofe amesema mshtakiwa alitenda kosa hilo January 3 mwaka huu maeneo ya namtanga jijini hapa.

Amemtaja mtoto aliyeuawa kuwa Steven Chinga ambaye alikuwa na umri chini ya miezi kumi na miwili kinyume na kifungu cha sheria namba 199 sura ya 16 kama kilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Hata hivyo mshtakiwa hakutakiwa kujibu lolote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na dhamana ya kusikiliza kesi kama hizo na kesi hiyo itaanza kusomwa upya februari 6 mwaka huu katika mahakama kuu.

MGOMO WA MADAKTARI HOSPITALI YA RUFAA, MBEYA NINI TAMATI YAKE?

Kamanga na Matukio | 04:26 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Mgomo wa madakta Hospitali ya Rufaa, Mbeya umeendelea huku madaktari hao wakidai kuwa mgomo huo utakuwa endelevu hadi hapo Serikali itakapo tekeleza madai yao.

Katika mgomo huo madaktari hao wamesema mgomo wao umelenga kuishinikiza Serikali kuboresha huduma za afya, kuowaongezea mshahara, posho na malipo ya kazi hatarishi pamoja na kuwapatia makazi kama ambavyo sheria ya nchi inavyoelekeza.

Akiongea na waandishi wa habari mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya Dokta Eliuta Sanker amesema mgomo huo umefanywa na madaktari wanafunzi 65 na madaktari wapya 10.

Mgomo huo wa madaktari ulianza January 23 mwaka huu baada ya mwenyekiti wa kamati ya muda wa jumuiya madaktari hao Stephano Ulimboka kutangaza mgomo usio na kikomo hadi madai yao yatakapotekelezwa

MAUAJI YA KUTISHA DHIDI YA WATOTO WAWILI MKOANI MBEYA

Kamanga na Matukio | 06:12 | 0 comments
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Nsenga jijini Mbeya wakitoka kushuhudia mwili wa mwanafunzi mwenzao wa darasa la Kwanza Silvia Isaya (5) alieuawa kisha viungo vya mwili wake kunyofolewa ulimi, jicho la upande wa kushoto, sehemu za siri na mguu wake wa kushoto kuvunjwa.
 Baadhi ya wananchi wa Nsenga jijini Mbeya wakishuhudia mwili wa mwanafunzi wa darasa la Kwanza Silvia Isaya (5) alieuawa kisha viungo vya mwili wake kunyofolewa ulimi, jicho la upande wa kushoto, sehemu za siri na mguu wake wa kushoto kuvunjwa.
 Mwili wa marehemu ilvia Isaya (5) alieuawa kisha viungo vya mwili wake kunyofolewa ulimi, jicho la upande wa kushoto, sehemu za siri na mguu wake wa kushoto kuvunjwa ukiwa umefunikwa kwa kitenge, kutokana na kuharibika vibaya hivyo kushindwa kuuonesha.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Nsenga Bwana Gibson Mwaselela (mwenye koti la rangi ya Samawati ), Baadhi ya wananchi wa Nsenga jijini Mbeya wakishuhudia mwili wa mwanafunzi wa darasa la Kwanza Silvia Isaya (5) alieuawa kisha viungo vya mwili wake kunyofolewa ulimi, jicho la upande wa kushoto, sehemu za siri na mguu wake wa kushoto kuvunjwa.(Picha na Ezekiel Kamanga, Mbeya).

Hitimisho:- Wimbi la mauaji dhi ya watoto limezidi kutanda mkoani  Mbeya baada ya watoto wawili kuawa katika nyakati tofauti  na watu wasiojulikana na kisha kunyofolewa sehemu za siri, ulimi na jicho la kushoto Wilaya ya Rungwe na Mbeya.

Kufuatia tukio hilo jumla ya wananchi 14 walikamatwa na Jeshi la polisi lakini machifu waliingilia kati, ambapo mtu mmoja aitwaye Joseph Mwangolobe (40 - 45) , mkazi wa Kiwira alijitokeza na kukiri kuwa ndiye aliyehusika na mauaji hayo chumbani kwake.

Jeshi la polisi lilifanya kazi ya ziada kumnusuru Joseph asiuawe na wananchi wenye hasira kali baada ya wananchi hao kutaka kulipiza kisasi, na familia yake imelazimika kuhama ikiwa chini ya ulinzi wa polisi.

Baba mzazi wa mtoto Silvia Isaya (5) Bwana Isaya Samson Mwalyego amesema alimwacha mwanawe Silvia majira ya saa 11:00 jioni Januari 13, mwaka huu alipokuwa anakwenda kazini Hoteli ya Silver Coin, hali mama yake akienda kutafuta mahitaji ya nyumbani kwa ajili ya mlo wa usiku.

Mama mzazi alipomaliza kupika alimtafuta mwanae pasipo mafanikio hivyo alitoa taarifa kwa mtendaji wa kijiji cha Nsenga Bwana Meshack Mwaipasi ambapo walitafuta usiku huo  bila mafanikio.

Asubuhi majira ya saa 2 kamili  Januari 24, mwaka huu mwili wa mtoto huyo ulipatikana katika shamba la mahindi Kitongoji cha Isenyela Kata ya Nsenga ukiwa umeondolewa baadhi ya viungo na mwili wa mtoto huyo ulichukuliwa na kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa kwa uchunguzi zaidi.

Kamanda wa Polisi Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba uchunguzi unafanyika ilikuweza kuwabaini waliohusika na tukio hilo la kikatili.


WANAWAKE WA KANISA LA MORAVIAN JIMBO LA KUSINI MAGHARIBI WAPEWA MSAADA WA MAJIKO NA TAA AMBAZO HUTUMIA MIOZI YA JUA

Kamanga na Matukio | 05:33 | 0 comments
 Idara ya Wanawake na watoto Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini Magharibi Tanzania limepokea misaada mbalimbali ikiwemo ya taa na jiko ambavyo vinazotumia miozi ya jua, ambapo msaada huo umetolewa na Kanisa la Moravian Ujerumani kwa ajili ya kuiwezesha idara hiyo kujikomboa kiuchumi.
 Jiko linalotumia miozi ya jua lenye thamani ya shilingi laki 5, lililotolewa na Kanisa la Moravian Ujerumani kwa ajili ya kuiwezesha Idara ya Wanawake na watoto kwa lengo kujikomboa kiuchumi, ambapo Jimbo hilo limepokea msaada wa majiko matatu na taa ishirini na tano, ambapo taa hiyo inakodishwa kwa shilingi elfu nne kwa mwezi..
Pichani ni Bi Ester Jonas Mwanzembe, akionesha bidhaa mbalimbali ambazo huzalishwa na wanawake wa Kanisa la Moravian Jimbo la Kusini Magharibi, ikiwa ni pamoja na virutubisho vya chakula na divai. 

Hitmisho:- Kanisa hilo limemteua mchungaji Lawrence Nzowa kwenda nchi ya Ethiopia kwa muda wa miezi miwili kwa lengo la kusomea taaluma ya utengenezaji wa taa na jiko ambapo vyote vinatumia miozi ya jua.

WATOTO YATIMA WASAIDIWA WILAYANI CHUNYA - MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:15 | 0 comments
 Waumini wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya wakipokea msaada hivi karibuni kutoka kwa Bi Sandra Witschi raia wa Uswisi, anayefanya kazi katika Jimbo hilo katika Idara ya Watoto na Wanawake.
 Bi Sandra Witschi akisisitiza watanzania kusaidia watoto yatima na kwamba watoto hao wakiendelezwa kielimu, nchi itaondokana na wimbi la ongezeko la watoto wa mitaani.
 Bi Sandra akiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima pamoja na walezi walioteuliwa kufuatilia maendeleo ya watoto hao kielimu, pamoja na maisha yao ndani ya jamii.
 Baadhi ya watoto 20 waliochaguliwa kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka huu wilayani Chunya, wakiwa katika picha ya pamoja na walezi wao baada ya kupokea msaada kutoka kwa Bi. Sandra Witschi hivi karibuni.(Picha na Ezekiel Kamanga, Chunya)

Hitimisho:- Bi Sandra Witschi ametoa msaada wa shilingi milioni 5.7 kwa watoto yatima wapatao 20, katika wilaya ya Chunya mkoani Mbeya kwa ajili ya kujiendeleza kielimu, fedha hizo zitatumika kwa ajili ya michango mashuleni, chakula pamoja na ada kwa mwaka mzima wa masomo.

Amesema kuwa zoezi hilo likifanyika kwa ufasaha litakuwa endelevu kwa watoto wengine na kisha ametoa ahadi ya kuwasomesha watoto hao mpaka kidato cha nne na wakifaulu wataendelea na masomo ya juu.

Bi Sandra ametaka jamii ya Kitanzania kuunga mkono mpango huo na kuwaimiza watoto yatima kupenda masomo yao na jamii kutowatumia kama watoto wa kazi za ndani.


WANANCHI WAONYWA KUACHA MARA MOJA KUTUMIA VIPODOZI HATARISHI.

Kamanga na Matukio | 02:35 | 0 comments
 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bwana Paul Sonda, katika mkutano mkuu wa madaktari wa Hospitali na zahanati binafsi katika mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Youth Centre  wa Roman Catholic jijini Mbeya.
 Mmoja kati ya madaktari waliohudhurua mkutano huo akivitambua baadhi ya vipodozi hatarishi na madhara yake, katika mkutano mkuu wa madaktari wa Hospitali na zahanati binafsi katika mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Youth Centre  wa Roman Catholic jijini Mbeya.
 Baadhi ya aina ya Vipodozi hatarishi kwa binadamu
 Vipodozi hatarishi kwa binadamu
Baadhi ya madaktari waliohudhuria katika mkutano mkuu wa madaktari wa Hospitali na zahanati binafsi katika mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Youth Centre  wa Roman Catholic jijini Mbeya.
Mganga mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya Dokta Seif Mhina, akizungumza na madaktari wa Hospitali na Zahanati binafsi katika Ukumbi wa Youth Centre uliopo katika Jiji la Mbeya.
*****
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Wananchi wametakiwa kuacha mara moja matumizi ya vipodozi hatarishi vilivyokatazwa na Mamlaka ya chakula na dawa nchini TFDA.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi mkuu wa Kanda ya nyanda za Juu kusini Bwana Paul Sonda, katika mkutano mkuu wa madaktari wa Hospitali na zahanati binafsi katika mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Youth Centre  wa Roman Catholic jijini Mbeya.

Ameviataja baadhi ya vipodozi kuwa ni MISS AFRICA, CITROLIGHT, COCODERM, CAROLIGHT, MAXLIGHT, EXTRA CLAIR, TOP LEMON PLUS, BETA SOL LOTION, LEMONVATE CREAM, JARIBU KWANZA, DIPLOSON, SUPER CLAIR, CLAIR MEN, FAIR AND HANDSOME, BIOCLARE, CAROTONE, MEDICATED FADE CREME, PRINCESS CLAIR, EPIDERM, BETASOL, IVAN HABART na SICAIRE.

Katika mkutano huo Bwana Sonda amesema kuwa watu wanaotumia vipodozi hivyo wanahatari kubwa ya kukumbwa na magonjwa ya kupoteza fahamu, kansa ya damu, kansa ya ini, ubongo, pia kwa akina mama wajawazito kujifungua watoto wenye mtindio wa ubongo, muwasho mwilini na kunenepa kupita kiasi.

Mbali na athari hizo hudidimiza uchumi kwa waathirika kutokana na gharama kubwa za kutibu na wengine kupoteza maisha au kupata ulemavu na kwamba amesikitishwa na wananchi hao kwa kung'ang'ania kuendelea kutumia vipodozi hivyo na kuvipitisha kwa njia ya panya.

Hivi karibuni Mamlaka ya Chakula na Dawa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato nchini waliteketeza vipodozi vyenye thamani ya shilingi milioni 129.

Hata hivyo Bwana Sonda amesikitishwa na kitendo cha wananchi wa Songwe ambapo vipodozi hivyo viliteketezwa baada ya kuchukua masalia ya vipodozi hivyo na kuvitumia.

MLINZI MBARONI KWA KUIBA SILAHA - MBEYA

Kamanga na Matukio | 01:41 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia Devid John mwenye umri wa miaka 36 mfanyakazi wa Kampuni ya ulinzi ya Simike kwa tuhuma za kuhusika na wizi.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi amesema mtuhumiwa huyo pamoja na wenzake wawili, Herman Davidi na Eriki Ismaili, wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi ya Kirumo  Security waliiba bunduki aina ya Shotigun Green yenye namba 565650 ambayo ni mali ya kampuni ya Kirumo.

Aidha Kamanda Nyombi ameongeza kuwa upelelezi zaidi kuhusiana na tukio hilo bado unaendelea.

WIMBI LA UBAKAJI LAZIDI KUSHAMIRI MKOANI MBEYA KIKONGWE ABAKA. - MBEYA

Kamanga na Matukio | 06:15 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Wimbi la ubakaji mkoani Mbeya limeendelea kushika kasi baada ya Mzee mwingine aliyefahamika kwa jina la Frank Mwakyeja (60 - 65), mkazi wa mtaa wa Ilolo B kata ya Isanga jijini Mbeya kuwabaka watoto wawili wa rika tofauti.

Tukio hilo limetokea Desemba 5, mwaka uliopita ambapo aliwabaka watoto hao wa jirani yake mmoja akiwa mwanafunzi wa Shule ya msingi Manga, jijini hapa mwenye umri wa miaka 9 na mwingine mwanafunzi wa shule ya msingi Madaraka jijini hapa mwenye umri wa miaka 7 (majina yao yanahifadhiwa).

Akizungumza na Mtandao huu Baba wa mmoja wa watoto walitendewa ukatili huo Bwana Gwakisa Mwakihaba (38), alifungua jarada la mashitaka MWJ/RB/270/2011, mnamo Desemba 6, mwaka jana na baadae jarada hilo kuhamishiwa Kituo kikuu cha Kati na kufunguliwa jarala namba MB/IR/10539/2011, ambapo mtuhumiwa alikamatwa na kuachiwa hali ambayo inapelekea hasira kwa wananchi iweje mtuhumiwa huyo aachiwe pasipo sababu maalumu.

Hata hivyo kwa mujibu wa wananchi hao waliokuwa na manung'uniko wamesema mtuhumiwa huyo anadaiwa kuwabaka watoto 6. mtaani hapo wakiwemo watoto mapacha, ambapo vitendo hivyo vimetafsiriwa kuwa nivya imani za kishirikina, hali ambayo ilipelekea wake wa mtuhumiwa huyo kukimbilia kwao mkoani Morogoro na mwingine Jijini Dar es salaam, kutokana na kuchoshwa na vitendo hivyo vya ubakaji vinavyotendwa na mume wao.

Watoto hao kwa pamoja wamefanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Wazazi ya Meta, Desema 6 na 7 mwaka uliopita na Daktari kubaini kuwa watoto hao walibainika kuingiliwa kimwili.

Kwa upande wake Bibi wa watoto hao Bi Ezelina Mwakihaba (70), amesikitishwa na kitendo cha mmoja wa wapelelezi wa kesi hiyo kuchelewesha uchunguzi na kutaka wafanye mazungumzo. licha ya familia ya mtuhumiwa kudai kutoa vitisho vya mauaji kwa hiyo.

HOSPITALI NA ZAHANATI BINAFSI ZIMEASWA KUTOTUMIA DAWA ZA SERIKALI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 06:14 | 0 comments
Mganga mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya Dokta Seif Mhina, akizungumza na madaktari wa Hospitali na Zahanati binafsi katika Ukumbi wa Youth Centre uliopo katika Jiji la Mbeya.
*****
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Hospitali binafsi zilizopo mkoani Mbeya zimeaswa kutotumia dawa za Serikali katika zahanati na hospitali ili kuepuka kufungiwa.

Hayo yamesemwa na Dokta Reinfredy Chombo wakati akitoa maada katika ukumbi wa youth centre jijini mbeya alipokutana na wamiliki wa hospitali hizo mwishoni mwa juma.

Chombo amesema katika ukaguzi kuna baadhi ya zahanati zimekutwa zikitoa dawa zilizoidhinishwa kwa matumizi ya hospitali za serikali hivyo kusababisha upungufu wa dawa katika hospitali hizo,na kuongeza kuwa kuna baadhi ya wahudumu katika hospitali hizo hawana vyeti na hivyo kufanya maisha ya wananchi kuwa mashakani.

Aidha Chombo amesema vituo vingi hapa mkoani havitumii kanuni za usafi na hivyo kuhatarisha afya za wagonjwa na kwamba wawe na tabia ya kujikagua wenyewe kabla ya kukaguliwa pia kutumia vifaa sahihi katika utabibu kwani kuna baadhi ya vituo vimekuwa vikitumiwa kutolea mimba hiyo ni kinyume na sheria ya nchi.

WILAYA YA MBEYA YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA MADARASA.

Kamanga na Matukio | 06:02 | 0 comments
Habari na Mtandao huu, Mbeya.
Wilaya ya Mbeya inakabiliwa na upungufu wa madarasa kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2012.

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Mbeya Evans Balama wakati akizungumza na bomba fm mwishoni mwa juma,balama amesema jiji la mbeya linakabiliwa na upungufu wa madarasa 59 wakati wilaya ya mbeya vijijini inakabiliwa na upungufu wa madarasa kumi na tano

Aidha Balama ameongeza kuwa wazazi wanawajibu wa kukamilisha madarasa hayo ili wanafunzi waweze kuanza masomo haraka iwezekanavyo ili ifikapo mwishoni mwa mwezi february madarasa hayo yawe yamekamilika ili wanafunzi waanze masomo haraka

Kwa upande wake afisa elimu mkoa wa mbeya Juma Kaponda amesema hawezi kutoa nafasi kwa wanafunzi ambao hawajapangiwa shule hadi watakapokamilisha ujenzi wa madarasa hayo huku akitolea mfano kwa kata ya iyela ina upungufu wa madarasa tisa na kusababisha zaidi ya wanafunzi 300 kukosa nafasi ya kupangiwa shule na hivyo kubaki nyumbani hadi sasa huku wenzao wakiendelea na masomo.

KAMATI NDOGO YAUNDWA KUHAMASISHWA MFUKO WA AFYA YA JAMII CHF WILAYANI RUNGWE - MBEYA

Kamanga na Matukio | 06:00 | 0 comments
Habari na Mtandao huu, Mbeya.
Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya imeunda kamati ndogo ya watu 10 itakayoandaa mikakati ya kuhakikisha hamasa ya mfuko wa afya ya jamii CHF inatolewa kwa wananchi ili waweze kujiunga kwa wingi.

Kamati hiyo imeundwa na mkuu wa wilaya Jackson Msome aliyekubaliana na wadau wengine waliohudhuria mkutano wa wakuu wa Idara za halmashauri hiyo wa kupata taarifa za maendeleo ya CHF na pia kujadili mradi mpya wa kuwasaidia wanawake wajawazito wasio na uwezo kupata huduma za matibabu chini ya utaratibu wa mfuko wa taifa wa bima ya afya NHIF.

Msome amesema ili kuhamasisha wananchi kujiunga kwa wingi ni lazima mikakati madhubuti iwekwe ikiwemo utoaji elimu kwa wakazi juu ya kuwa na bima itakayowahakikishia huduma ya afya pale wanapopata matatizo ya magonjwa.

Awali akizungumzia sababu za wananchi waliokuwa wamejiunga na mfuko huo kujitoa,mganga mkuu wa wilaya Dokta Sungwa Ndagambwene alisema baadhi walikatishwa tama na kasoro zilizobainika ikiwemo uhaba wa dawa jambo ambalo alisema hivi sasa limewekewa mikakati tofauti na kipindi hicho.

MTU MMOJA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA UBAKAJI

Kamanga na Matukio | 05:57 | 0 comments
Habari na Mtandao huu, Mbeya.
Robert John Hasani mwenye umri wa miaka 24 mkazi wa Majengo jijini Mbeya amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mbeya kwa kosa la ubakaji.

Akisoma shtaka hilo mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo Monika Ndyekobora mwanasheria wa Serikali Fransisi Rojasi amesema disemba 25 mwaka jana mshatakiwa alimbaka mwanamke mwenye umri wa miaka 36 kinyume na kifungu cha sheria namba 130 B na kifungo 131 sura ya kwanza ya marekebisho ya mwaka 2002.

Mstakakiwa amerudishwa rumande kwa kutokidhi masherti ya dhamana ambapo dhamana ni shilingi milioni mbili na kwamba kesi hiyo itasomwa tena Februari pili mwaka huu.

Siku hiyo hiyo Eva Mwakibinga mwenye umri wa miaka 24 mkazi wa Makunguru amefikishwa katika mahakama hiyo ya mkoa kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi wifi yake.

Mwanasheria wa Serikali Fransisi Rojasi amesema mshtakiwa ametenda kosa hilo la kumpiga, kumng'ata Fransiska Ediani na kumsababishia maumivu shavu lake la kushoto kinyume na kifungo cha sheria namba 225 sura ya 16, hata hivyo hakimu Monika Ndyekobora ameihairisha na huku ya kesi hiyo itatolewa Februari pili baada ya mshtakiwa kukiri kutenda kosa hilo.

KILA KUKICHA VITENDO VYA UBAKAJI VYAZIDI KULITIKISA JIJI LA MBEYA.

Kamanga na Matukio | 05:49 | 0 comments
Habari na mwandishi wetu.
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Jamesi mwenye umri wa miaka 40 amenusurika kifo baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira kali akituhumiwa kumbaka binti mwenye umri wa miaka 16 makazi wa kata ya Ilemi jijini Mbeya.

Tukio hilo limetokea jana majira ya saa mbili za asubuhi ambapo mtuhumiwa huyo aliingia nyumbani anakoishi binti huyo wakati akiwa peke yake na kuanza kumuingilia kimwili bila ridhaa ya mwanamke huyo.

Wakazi wa eneo hilo walipata taarifa ya kubakwa kwa binti huyo baada ya kusikia kelele zikitoka ndani ya nyumba na kwamba baada ya kufika walimkuta kijana huyo akimwingia kimwili binti huyo ambAye tumemuhifadhi jina kwa sababua za kimaadili.

Mama mzazi wa mtoto huyo amesema kuwa mwanae ameingiliwa kimwili na kijana huyo wakati yeye akiawa katika biashara zake ndogondogo.

Kwa upande wake balozi wa mtaa huo wa Ilemi darajani khamadi mwakajinga amesema pamoja na mtuhumiwa kukamatwa wananchi waliafikiana kumwachia kijana huyo kutokana na kile alichokieleza kuwa mtuhumiwa ametoa gerezani hivi karibuni kwa msamaha wa Rais.

KIKONGWE MBAKAJI AFIKISHWA MAHAKAMANI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:47 | 0 comments
 Baba mzazi wa binti aliyebakwa na Mzee Asangile Kihaka (70), anayefahamika kwa jina la Bwana Ekson Nazareth  (47), ambaye pia ni mzee wa baraza mahakama ya Mwanzo ya Mbeya Mjini.. 
 Mmoja wa wananchi wa eneo la Ghana akilaani vikali kitendo cha Mzee Asangile Kihaka (78) kumbaka binti wa miaka 12, mwanafunzi wa darasa la 7 katika Shule ya Msingi Mbata, ambapo ni tukio la tatu la mzee huyo kutenda.
******
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mzee Asangile Kihaka mwenye umri wa miaka 75 mkazi Ghana amefikishwa katika mahakamani ya hakimu mkazi mkoa wa Mbeya jana akituhumiwa kumbaka mtoto wa miaka 12 disemba 14 mwaka jana.

Akisoma shtaka linalomkabili mzee huyo mwanasheria wa Serikali Roda Ngole mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Zabibu Mpangule amesema mzee Asangile alitenda kosa hilo akiwa nyumbani kwake baada ya kumrubuni mtoto huyo kumpelekea kuni nyumbani kwake na baada ya mtoto kufika ndani mzee huyo alianza kumwingilia kimwili kwa nguvu.

Amesema kitendo hicho ni kinyume cha kifungo cha Sheria 130 sura ya pili E na kifungu namba 131 sehemu ya kwanza sura ya 16 marekebisho ya mwaka 2002.

Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Zainabu Mpangule ameihairisha kesi hiyo hadi February mosi mwaka huu na kwamba mtuhumiwa amerudishwa rumande baada ya kukosa dhamana ya shilingi laki tano.

RAIA 27 WA SOMALIA WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI KINYUME NA SHERIA - MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:41 | 0 comments
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi.
***** 
Habari na Mwandishi wetu.
Raia 27 wa Somalia wanashikiliwa na Jeshi la polisi mkoa wa Mbeya kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha Sheria.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amesema kuwa raia hao wa kigeni wamekamatwa jana maeneo ya Nonde jijini hapa wakati polisi wakiwa katika doria.

Amesema kati ya raia hao mmoja ndiye aliyeweza kujitambulisha kwa jina Genesis Basema mwenye umri wa miaka 26 na kuongeza kuwa raia hao walikuwa wakiishi kwenye pagara kwa muda usiojulikana.

Wakati huohuo Kamanda Nyombi ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la polisi pindi wanapokuwa na taarifa ya kuwepo kwa raia wowote wa kigeni hapa nchini ili kudhibiti vitendo vya uvamizi.

NYETI ZA MWANAMKE ZATOWEKA USINGIZINI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 05:32 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Tunkumbukege Mbalaswa (20) mama wa watoto wanne mkazi wa kijiji cha Nsongola kata ya Bujela wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya amekuwa kwenye wasiwasi baada ya sehemu zake za siri kutoweka usiku wa Desemba 30 mwaka uliopita.

Akiongea kwa masikitiko Bi  Tunkumbukege amesema alijifungua salama kabisa mtoto wa kiume October 2011 aitwaye Shaban Elia na hakupatwa na tatizo lolote hadi Desemba 30, mwaka jana alipokutwa na tatizo la sehemu za siri zikiwa zimeondolewa hali iliyomsababishia maumivu makali na hivyo kumlazimu kwenda Zahanati ya Bujela na kuonana na Daktari wa zahanati hiyo na kumpata dawa mama huyo akidai ni ugonjwa wa Fistula.

Baada ya siku saba za matibabu kumalizika hali ya mwanamke huyo iliendelea kuwa mbaya huku sehemu zake za siri zikionekana zimekeketwa na tundu la mkojo kutobolewa na spoko ya baiskeli hali ambayo haja ndogo ikimtoka bila utaratibu na kupata hadha kubwa.

Bi  Tunkumbukege Mbalaswaalijifungua mtoto wa kwanza mwaka 1997, na mtoto wa pili mwaka 2003 wote wakiwa ni jinsi ya kike, mtoto wa tatu mwaka  2006 na mtoto wa kiume mwaka 2011 wote wakiwa ni jinsi ya kiume ambapo wote hajapata matatizo yoyote katika uzazi.

Kwa upande wake Mumewe Bwana Elia Mwambapa amesema matatizo yote amemwachia Mungu kwani mkewe amekuwa akipata shida licha ya kumaliza dawa, mkewa hajapata hafueni yoyote.

Uchunguzi uliofanywa na Daktari amesema katika utabibu wake hajawahi kukumbana na mgonjwa mwenye tatizo hilo  na kwamba baada ya vipimo vya Fistula amegundua kuwa mgonjwa wake hana ugonjwa huo(Fistula).

Kufuatia hali hiyo Bi Tunkumbukege anahusisha tatizo hilo na imani za kishirikina hali ambayo imepelekea kupatiwa matibabu na mganga wa tiba za asili(jadi)ambaye hakupenda kumtaja jina.

Mkoa wa Mbeya ni moja ya mikoa ambayo imekuwa ikihusishwa kutawaliwa na imani za kishirikina, hali ambayo imepelekea wakazi wake kuendelea kuishi kwa hofu, kutokana na baadhi ya watu kuendekeza kuishi katika imani hizo na wengine kuuawa na wananchi wenye hasira kali.

WIMBI LA UBAKAJI MAUAJI:- WATU WAWILI WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MATUKIO MAWILI TOFAUTI - MBEYA

Kamanga na Matukio | 07:00 | 0 comments
Habari na Mwandishi wetu.
John Jackson mwenye umri wa miaka 19 mkazi wa Mbeya Pick amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mbeya kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 12 maeneo ya Mbeya Pick.

Akisoma shtaka hilo mwanasheria wa Serikali Faraja Msuya mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Monica Ndyekobora amesema mshtakiwa alimbaka mtoto huyo disemba 21 mwaka jana katika maeneo ya Mbeya Pick.

Amesema kuwa kitendo hicho ni kinyume cha kifungu cha Sheria namba 130 kifungu cha pili E na kifungu cha 131 sura ya 16 marekebisho ya mwaka 2002.

Hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa hadi January 31 mwaka huu na mtuhumiwa amerudishwa rumande kwa kukosa dhamana.
 
Wakati huohuo Fransis Anyosisye Mwakatika mkazi wa Soko matola jijini Mbeya amefikishwa katika mahakama ya hakimu makazi mkoa wa Mbeya kwa kosa la mauaji eneo la Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini.

Akisoma shtaka hilo Mwanasheria wa Serikali Adolfu Maganda mbele ya Hakimu mkazi wa mahakama hiyo Kusaga Majinge amesema kuwa mshtakiwa Fransis Mwakatika alimuuwa Fred Manji mwezi disemba mwaka jana.

Kitendo hicho ni kinyume cha Sheria kifungu namba 196 sura ya 16 marekebisho ya mwaka 2002.

Hata hivyo mshtakiwa hakuruhusiwa kujieleza chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na dhamana ya kusikiliza kesi hiyo, na kwamba mahakama kuu pekee ndiyo yenye dhamana ya kusikiliza kesi hiyo.

MGOGORO KATI YA WAKULIMA, WANAKIJIJI NA MWEKEZAJI HALI NI TETE - MBEYA

Kamanga na Matukio | 06:57 | 0 comments


Mfugaji Bwana Mungo Makubi (27) kushoto na Singu Mwakami (23) wakimtazama ng'ombe aliyeuawa kwa kugongwa na gari aina ya Toyota Landcruiser  lenye nambari ya usajili T 566 BQH. iliyokuwa ikiendeshwa na mwekezaji wa Kapunga Rice Project wilayani Mbarali aitwaye Bwana Gerry Baquzein baada ya kuwakosa wafugaji hao baada ya kujistiri nyuma ya mti na kisha hasira za mwekezaji kuishia kwa kumgonga ng'ombe huyo mwenye thamani ya shilingi laki 6 za kitanzania na kisha kufa papo hapo. 
*****
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mgogoro kati ya wakulima, wanakijiji na mwekezaji wa shamba la Kapunga kampuni ya Export Traders lililopo wilayani Mbarali mkoani Mbeya huenda ukawa endelevu kutokana na Serikali kushindwa kutolea ufafanuzi hatma ya mgogoro huo ambao umekuwa ukiwasababishia wanakijiji wa Kapunga kujeruhiwa na kukosa haki zao za msingi.

Utata wa kumalizika kwa mgogoro huo umetokana na Waziri wa kilimo na Chakula ushirika Profesa Jumanne Maghembe kushindwa kuzungumza lolote pindi alipoombwa na waandishi wa habari kuzungumzia hatma ya mgogoro huo.

Wanahabari walilazimika kumtaka Waziri Maghembe kuzungumzia suala hilo baada ya kutoa kauli katika kikao cha wakulima wa zao la kahawa na viongozi wa Serikali mkoani Mbeya kuwa viongozi wanatakiwa kusimamia vyema bei za mazao badala ya kuwaachia walanguzi wakiendelea kuwanyonya wakulima.

Hivi karibuni Mwekezaji wa Kapunga Rice Project amekuwa akiwanyanyasa wakulima wa zao la mpunga kwa kuwapiga viboko, kuwasababishia majeraha mbalimbali kwa kuwagonga na gari ikiwa ni pamoja na kuuwa mifugo yao huku mwekezaji huyo akiachwa bila ya kuchukuliwa hatua zozote za kisheria.

WAZIRI MAGHEMBE - SIWEZI KUPINGA UAMUZI WA VIONGOZI WA MKOA KUZUIA UUNZWAJI WA KAHAWA MBIVU.

Kamanga na Matukio | 06:55 | 0 comments
Waziri wa Chakula, Kilimo na Ushirika Profesa Jumanne Maghembe.
******
Habari na Mwandishi wetu.
Waziri wa kilimo chakula na Ushirika Profesa Jumanne Maghembe amesema kuwa hawezi kupinga maamuzi ya viongozi wa wilaya za Mbeya, Ileje, Rungwe na Mbozi kuhusu uamuzi wa kupinga biashara ya uuzaji wa Kahawa Mbivu. 

Amesema kuwa hawezikutengua kanuni za Wizara na Bodi ya kahawa juu ya ununuzi wa kahawa mbivu na kuitaka Serikali mkoani Mbeya kusimamia sheria na kuhakikisha bei kwa wakulima wa kahawa zinakuwa nzuri ili wakulima waweze kunufaika kupitia kilimo chao.

Naye mkurugenzi wa bodi ya kahawa nchini Adolph Kumbulu na mwanasheria wa Wizara ya kilimo amesema kuwa ununuzi wa kahawa mbivu umeongeza tija ya ubora wa kahawa Tanzania kutokana na ubora wa usindikaji wake tofauti na usindikaji unaofanywa na wakulima.

Kwa upande wao viongozi wa mkoa wa Mbeya walisimama katika masimamo wao wa kutoruhusu uuzaji wa kahawa Mbivu kwani umelenga kuwanyonya wakulima wadogo wadogo.

CHAMA CHA MASOKO MKOANI MBEYA KIMEUTAKA UONGOZI WA HALMASHAURI YA JIJI KUTOWANYANYASA WAFANYABIASHARA.

Kamanga na Matukio | 06:44 | 0 comments
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Bwana Evans Balama(kushoto) akiwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbeya maarufu kama Ndomboro, katika moja ya vikao vya kujadili masuala mbalimbali ya kutatua kero za wakulima .(Picha na Maktaba yetu)
******
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Chama cha wafanyabiashara wa masoko jijini Mbeya kimeutaka uongozi wa Halmashauri ya jiji kutowanyanyasa wafanyabiashra hao kutokana na viongozi wa jiji kupandisha ushuru kiholela bila makubaliano baina yao.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa chama hicho Bwana Charles Syonga alipokuwa akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari mkoani Mbeya katika ukumbi wa Chuo cha Wafanyakazi (OTTU), eneo la Kabwe jijini hapa.

Ameyasema hayo kufuatia halmashauri ya jiji kupandisha ushuru kwa wafanyabiashara hao kutoka shilingi 200 hadi shilingi 500 kwa siku kwa wafanyabiashara wanaopanga bidhaa zao mezani, na shilingi kutoka 15,000 hadi shilingi 65,000 kwa mwezi kwa vizimba na nyumba katika masoko ya Uhindini, Sido Mwanjelwa, Soweto, Ikuti, Airport, Mabatini, Isanga, Uyole, Igawilo na Soko matola.

Kufuatia tamko hilo kwa tangazo la halmashauri ya jiji lililotolewa Januari 6 mwaka huu, ambalo limebandikwa maeneo mbalimbali ya jiji na utekelezaji wake kuanza Januari 16 mwaka huu hali iliyoleta mtafaruku katika utekelezaji wake na kisha kusababisha wafanyabiashra wa soko la Ikuti na Soweto kugoma kulipa ushuru huo na kukataa kuingia sokoni kupanga bidhaa zao.

Sakata hilo limepelekea Mkuu wa wilaya ya Mbeya Mheshimiwa Evans Balama kuingilia kati na kumuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Mbeya Bwana Juma Iddi kulitatua tatizo hilo mara moja, agizo alilolitoa Januari 16 mwaka huu.

Baada ya mgomo huo wa wafanyabiashara uliodumu kwa takribani saa tatu baada ya uongozi wa jiji kukubali ushauri wa Mkuu wa wilaya , hali iliyopelekea wafanyabiashara hao kuendelea kulipia ushuru wa awali.

Bwana Syonga wafanyabiashara wengi wao wana mitaji midogo kuanzia shilingi 5,000 hivyo kitendo cha kuwalipisha ushuru wa shilingi 500ni sawa na kudidimiza maisha ya wajasiriamali wa jiji kutokana na uongozi wa jiji kushindwa kuboresha miundombinu ya masoko yote na kushindwa kufanya usafi katika mazingira yanayowazunguka wafanyabiashara hao.

Akienda mbali Bwana Syonga amesema wafanyabiashara waengi wamekuwa wakipata huduma ya choo cha kulipia  kwa gharama ya shilingi 200 na endapo biashara siku hiyo itatetereka , mafanyabiashara anaweza kutumia shilingi 600, hivyo mwisho wa siku kurudi nyumbani akiwa hana kitu.

Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu umebaini kuwa halmashauri ya jiji imekuwa ikikusanya shilingi milioni 260, kwa mwaka kutokana  na ushuru huo wa shilingi 200, pesa ambayo ni nyingi ukilinanisha na huduma anayopewa mfanyabiashara.

Hata hivyo Mkurugenzi wa Jiji Bwana Juma Iddi hakuwa tayari kuzungumzia lolote, na kwamba atatoa tamko lake leo katika ofisi za halmashauri ya jiji.

MGOMO WA MADEREVA WA MALORI WAENDELEA - TUNDUMA

Kamanga na Matukio | 06:05 | 0 comments
Katikati mwenye koti jeusi diwani wa kata ya Tunduma Mheshimiwa Frank Mwakajoka Baada ya wafanyabiashara kushindwa kufanyabiashara zao na kupelekea kufunga kutokana na vurugu zilizotokea za kupingwa ucheleweshaji wa matokea ya uchaguzi nchini Zambia sasa ni shwari na wananchi wameanza kuvuka mpaka na wafanyabiashara kurejea katika shughuli zao.
 
Madereva wakielekea kukamilisha ushuru wa forodha na kukamilisha taratibu za kuvuka mpaka kuelekea nchini Zambia na Kongo. (Picha kutoka Maktaba yetu)
 *****
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Siku ya tatu mfululizo madereva wa magari ya mizigo wameendelea kugoma katika mji mdogo wa Tunduma mkoani Mbeya, kutokana na waajiri wao kutofanyia kazi madai yao.

Baadhi ya madai ya madereva hao ni pamoja na kulipwa mishahara midogo, kunyimwa pesa za kujikimu safarini, kutokuwa na makato ya mafao ya uzeeni.

Madereva hao wameamuka kutovuka mpaka pia kuingia nchini kwa madai ya kupatiwa ajira ya kudumu na waajiri wao suala ambalo liliingiliwa kati na Waziri wa Uchukuzi Omar Nundu mwishoni mwa mwaka jana, jambo ambalo waziri huyo aliahidi kulitatua suala hilo

Kutokana na msongamano wa magari hayo kumepelekea shughuli za kiuchumi kudhorota katika mji wa Tunduma kwani wengi wamekuwa wakitegemea wageni kutoka nchi za kusini mwa Afrika kama vile Congo, Botswana, Zimbabwe, Lesotho, Namibia na Afrika Kusini ambao wengi hutegemea mpaka wa Tunduma kupitishia bidhaa zao.

Mbali na usumbufu huo Diwani wa mji mdogo wa Tunduma Mheshimiwa Frank Mwakajoka amesema ajali nyingi zimekuwa zikitokea kutokana na msongamano huo, pia wakazi wengi wamelazimika kutembea kwa miguu kutokana na magari kushindwa kupita katika barabara ya Tunduma/Sumbawanga na Tunduma/Mbeya.

Aidha Mwakajoka amesema uchafuzi wa mazingira umekuwa ukifanywa na madereva hao kutokana na kukosa pesa za matumizi hivyo kukosa malazi hali inayowalazimu kujisitiri chini ya uvungu wa magari.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mbozi Gilbert Kimoro amesema wamechukua tahadhari ya kuandaa gari la wagonjwa kutokana na hofu ya mlipuko wa magonjwa, ili kukabiliana na lolote linaloweza kutokea .

Wakati huo huo Kimoro amesema kuwekuwa na hofu ya usalama kutokana na madereva hao kutosafiri na muda mwingi kuwepo mahali pamoja hali inayoweza kuleta uvunjifu wa amani, pia amebainisha hivi sasa madereva wameanza kujaza fomu zilizotolewa na SUMATRA, ingawa madereva hao wamesema pamoja na kujaza fomu hizo hawataweza kuendelea na safari.

Amesema suala hilo limecheleweshwa na madereva hao kutokana na mchakato wa katiba wa madereva hao ambao ulianza mwaka uliopita.

Ili kuhakikisha amani inakuwepo Tunduma, Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi amepiga kambi mpakani hapo kwa siku mbili mfululizo ili kuhakikisha amani na utulivu mpakani pia kuhakikisha usalama wa raia na mali zao.

KABURI LAFUKULIWA BAADA YA POLISI KURUHUSU KUZIKA KWA TUHUMA ZA WIZI.

Kamanga na Matukio | 05:38 | 0 comments
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbozi.
Jeshi la polisi mkoani Mbeya limeingia lawamani baada ya wananchi mbalimbali kulalamikia utendaji kazi wa Jeshi hilo baada ya kukumbatia vitendo vya kihalifu vinavyofanywa wilaya ya Mbozi, mkoani Mbeya, kutokana na kukinzana na dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi.

Mnamo Januari 15, mwaka huu siku ya Jumapili, Jeshi la polisi kutoka Kituo cha Mlowo wilayani Mbozi walilazimishwa kufukua kaburi la kijana mkazi wa Msiha aliyeuawa hivi karibuni kwa tuhuma za wizi wa debe moja la karanga mali ya Sengo, katika kitongoji cha Nyelya, kijiji cha Hatelele na kisha kuchomwa moto na kuzikwa bila ndugu zake kufahamu, huku jeshi hilo likishindwa kuwakamata waliohusika na mauaji hayo.

Baada ya ndugu wa marehemu kupata taarifa za ndugu yao kuuawa walikwenda mahakamani kupata kibali cha kufukua mwili huo ambao ulifukuliwa majira ya saa 7 mchana na kwenda kuzikwa katika kijiji cha Msiha.

Kituo cha Mlowo ni moja ya kituo kinacholalamikiwa na kwa kusababisha mauaji kwa watu wanaouhumiwa kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya wizi, ambapo Mkuu wa kituo hicho kuagizwa kuwa mhalifu afikishe kituoani hapo akiwa ameuawa na sio hai.

Hayo yamethibitishwa na Mwenyekiti wa haki za Binadamu wa wilaya hiyo Bwana Bruno Mwambene na kuthibitishwa na mwenyekiti wa mkoa Bwana Said Madudu ambapo walionesha nyaraka mbalimbali za malalamiko ya wananchi ambao ni ndugu wa watu waliouawa.

WAFANYABIASHARA WA SOKO LA SOWETO JIJINI MBEYA WASITISHA MGOMO

Kamanga na Matukio | 05:11 | 0 comments
Taswira ya baadhi ya vibanda na bidhaa ya nyanya katika Soko la Soweto Jijini Mbeya.
*******
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Wafanyabiashara wa soko la Soweto Mbeya wamesitisha mgomo baada ya kuafikiana na halmashauri ya jiji la Mbeya kuhusu kupunguza ushuru wa biashara.

Mgomo wa wafanyabishara hao ulianza leo hii majira ya saa moja za asubuhi na ulidumu kwa muda wa masaa matatu, hata hivyo majira ya saa 4 za asubuhi wafanyabiashara hao waliendelea na biashara zao kama kawaida.

Wakiongea na mwandishi wetu baadhi ya wafanyabishara wa soko la Soweto walisema kupanda kwa kiwango cha ushuru kutoka shilingi mia mbili hadi mia tano, ni kikubwa na wao hawawezi kukabiliana nacho kutokana na kipato chao kuwa kidogo.

Kwa upande wake mkurugenzi wa jiji la Mbeya Juma Iddi alipoongea na mwandishi wetu kuhusu sakata hilo alisema kuwa mazungumzo kati ya uongozi wa Soko na Serikali yanaendelea vizuri na kwamba atatolea ufafanuzi mara baada ya kikao kumalizika.

Wakati huohuo tumepata taarifa kuwa madereva wa magari ya mizigo yafanyayo safari zake ndani na nje ya nchi wameanza mgomo wakidai kuwepo kwa usarasimu wa kuvuka mpaka wa Tanzania na Zambia katika upande wa Tanzania.
 
Naye Mkuu wa wilaya ya Mbeya Bwana Evans Balama amesema kuwa jiji linapaswa kukaa na wafanyabiashara hao ili kufikia muafaka, ili maamuzi yao yasiwaathiri wateja.
 
Hata hivyo mgomo huo wa wafanyabiashara umekuja mara baada ya Halmashauri ya jiji kupandisha ushuru kutoka shilingi 200 hadi shilingi 500, kwa wateja waliokuwa wakipanga bidhaa zao mezani na kwa vyumba kutoka shilingi 15,000 hadi kufikia 65,000 licha ya soko hilo awali kukosa wateja.

WAZIRI MAGHEMBE ZIARANI MBEYA AKUTANA NA WAKULIMA WA ZAO LA KAHAWA - MBOZI

Kamanga na Matukio | 05:01 | 0 comments


 Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Profesa Jumanne Maghembe.
*****
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Profesa Jumanne Maghembe leo hii amekutana na wakulima wa zao la kahawa kutoka wilaya za Mbeya, Mbozi, Rungwe na Ileje kwa ajili ya kujadili mstakabali wa zao la kahawa.

Akiwa wilayani Mbozi, baadhi ya wakulima wa zao la Kahawa ambao walizuiwa kuhudhuria mkutano huo waliusimamisha msafara wa waziri Maghembe ikiwa ni ishara ya kushinikiza uongozi wa halmashauri kuwaruhusu kushiriki kwenye mkutano huo.


Baada ya tukio hilo mkuu wa mkoa wa Mbeya Bwana Abbas Kandoro aliwataka wakulima hao kuwachagua wawakilishi wao ambapo kila kikundi kiliwakilishwa na wajumbe wawili kushiriki katika mazungumzo hayo, lakini Mkuu wa mkoa huyo aliwataka wakulima kuteua wakulima kumi kuingia katika mkutano huo .

Katika mkutano huo baada ya kutokea mvutano mkubwa juu ya ununuzi wa kahawa mbivu na kavu Waziri Maghembe alikubaliana na uongozi wa mkoa wa Mbeya kwamba hawezi kutengua maamuzi yaliyoamuliwa ya kupiga marufuku ununuzi wa kahawa mbivu(cherry).
Awali wakulima wa zao la Kahawa wilayani Mbozi walikuwa wakiilalamikia Serikali kutoa upendeleo kwa makampuni yanayohusika na ununuzi wa kahawa na vikundi vinavyodaiwa kuwa ni vya vigogo ambavyo ndivyo vimetajwa kuhusika na urasimu licha ya mkulima kuendelea kuteseka kutokana na kukosa pembejeo za kisasa na hivyo kupata hasara kubwa ya kutunza kahawa.
Katika mjadala huo mwanasheria wa Wizara ya kilimo na ushirika alisema sheria inaruhusu kununua kahawa mbivu na ndio maana kikatolewa kibali kwa kampuni ya Lima kuendelea na ununuzi wa kahawa mbivu, ambapo kampuni hiyo ilikuwa ikiwasaidia wakuliwa kuwakopesha pembejeo. 

Wakati huohuo wakulima walishindwa kufahamu kilichoendelea kutokana na uongozi wa mkoa na wilaya kuwa wasemaje wakuu wa mkutano badala ya wakuliwa ili kutoa changamoto zao.

Aidha kuhusiana na Sakata la mwekezaji wa Kapunga Rice Project wilayani Mbarali Waziri Maghembe alipoulizwa na waandishi wa habari nje ya mkutano alishindwa kulitolea majibu na kudai kuwa atakuja kwa awamu nyingine ili kulizungumzia.

Alipoulizwa kuwa Je?, ana mkakati gani kuhusiana na wawekezaji kuua mifugo ya wafugaji na kufunga njia zote zianazoingia na kutoka shambani hapo, ambazo hutumiwa na wananchi katika shughuli zao za kiuchumi, Waziri Maghembe alisema haelewi chochote na wala hajapewa taarifa.
 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger