Wanafunzi wa shule ya msingi Nero Jijini
Mbeya wako hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na hali ya vyoo
wanavyotumia.
Hayo wameyasema hii leo wakati walipokua
wakizungumza na mwandishi wetu wamesema hali ya vyoo shuleni hapo ni mbaya
kutokana na kujaa kwa takribani miezi
saba hali inayowafanya kujisaidia vichakani na wengine kujisaidia pembeni ya
tundu la choo.
Mmoja wa wanafunzi hao Memori Kiandu amesema
wamekuwa wakisumbuliwa na hali hiyo licha ya kuchangia shilingi elfu tatu kwa
ajili ya kujengewa vyoo vingine.
Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Gasper
Lyimo amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na
kusema mamlaka husika isimamie suala hilo
kwani limedumu kwa muda mrefu.
Hata hivyo mwenyekiti wa mtaa wa Iyela Two Pipingu
Mwakilasa amesema wameanza kujenga vyoo vingine kutokana na kujaribu kuzibua
vyoo hivyo na kushindikana.
0 comments:
Post a Comment