Na Shaban Kondo,
Kamati ya Rufani ya
Uchaguzi ya Shirikisho la soka nchini TFF imeahidi wadau wa mchezo huo itafanya
kazi zake kwa misingi ya haki katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi
mku wa TFF utakaofanyika jijini Dar es salaam Februari 24.
Mwenyekiti wa kamati
hiyo iliyoundwa baada ya waraka wa mabadiliko ya katiba ya TFF kupitishwa na
wajumbe wa mkutano mkuu mwishoni mwa mwaka jana Idd Mtiginjola amesema kamati
yake itasimamia misingi ya haki kwa kuvitafsiri vifungu vya katiba pamoja na
kanuni za uchaguzi endapo rufaa iltawasilishwa kwao.
Awali katibu mkuu wa
shirikisho la soka nchini TFF Angetille Osiah aliitambulisha kamati hiyo ya
rufaa kwa waandishi wa habari na kutoa sababu za kuundwa kwa kamati hiyo itakua
ikifanya kazi zake kwa mara ya kwanza baada ya kuingizwa katika mchakato wa
uchaguzi wa mwaka huu.
Amesema sababu za
kuundwa kwa kamati hiyo ni kutaka kutanua wigo wa kupatikana kwa haki pale
litakapojitokeza masuala ya utata kama ilivyokua siku za nyumba ambapo kamati
ya uchaguzi ilikua inajibebesha majukumu ambayo yalikua si halali kwake.
Baada ya utambulisho
huo Angetille Osiah aliwakabidhi wajumbe wa kamati hiyo vitendea kazi mbalimbali zikiwemo kanuni za uchaguzi za TFF
na wanachama wake, Katiba ya TFF na Katiba ya Shirikisho la soka la Kimataifa
la (FIFA).
Mbali ya Iddi Mtiginjola,
wajumbe wengine wanaounda kamati hiyo ni Makamu Mwenyekiti, Francis Kabwe
ambaye ni Naibu Msajili wa Mahakama Rufani ya Tanzania, Kamanda wa Kikosi cha
Usalama Barabarani Tanzania, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP),
Mohamed Mpinga ambaye pia kitaaluma ni Mwanasheria.
Mshambuliaji wa zamani
wa timu ya Reli Morogoro, Profesa Madundo Mtambo ambaye kwa sasa ni Mkufunzi
katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kilichopo mjini Morogoro, na
mdau wa soka Murtaza Mangungu ambaye pia ni Mbunge wa Kilwa Kaskazini.
0 comments:
Post a Comment