Kiungo wa klabu ya Manchester
United, Shinji Kagawa ameitwa tena
katika kikosi cha timu ya taifa ya Japan kitakachocheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki
dhidi ya timu ya taifa ya Latvia utakaochezwa kati kati ya juma lijalo.
Shinji Kagawa ameitwa
kwenye kikosi cha Japan ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu mwishoni mwa mwaka
jana ambapo ilishuhudiwa akiukosa mchezo wa kusaka nafasi ya kucheza fainali za
kombe la dunia dhidi ya timu ya taifa ya Oman ambayo ilikubali kuchapwa mabao
mawili kwa moja.
Kwa kipindi kirefu kiungo huyo
mwenye umri wa miaka 23, alikua nje akiugulia maumivu ya nyama za paja kabla ya
kurejea mwezi Disemba mwaka jana na kuonyesha kiwango wakati wa mchezo wa ligi
kuu ya soka nchini Uingereza dhidi ya Man city ambao walikubali kichapo cha
mabao mawili kwa moja.
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Japan
Alberto Zaccheroni amesema amekuwa
akimfuatilia nyota huyo katika michezo kadhaa aliyocheza na hivyo ameshawishika
kumuitwa kwenye kikosi chake baada ya kurejea katika kiwango chake cha kawaida.
Kiungo mshambuliaji wa klabu ay Cardiff City Craig Douglas Bellamy amerejeshwa kwenye kikosi cha
timu ya taifa ya Wales ambacho kinakabiliwa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki
dhidi ya timu ya taifa ya Austria utakaochezwa kati kati ya juma lijalo mjini
Swansea.
Craige Bellamy
mwenye umri wa miaka 33, amerejeshwa kikosini baada ya kukosa michezo minne ya
kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia lakini uwezo na kujituma kwake
kumemfanya kocha mkuu wa timu ya taifa ya Wales Chris Coleman kumtaja katika kikosi chake.
Kwa mara ya mwisho Craige Bellamy aliichezea
timu ya taifa ya Wales mwezi August mwaka jana wakati wa mchezo dhidi ya Bosnia-Herzegovina ambao walichomoza na
ushidni wa mabao mawili kwa sifuri.
Chris Coleman
amesema kumrejesha Bellamy kikosini
pia kutaongeza nguvu kwa wachezaji chipukizi ambao wanataka kujifunza kupitia
kwa goji huyo, hivyo ana matarajio makubwa kwa kiungo huyo kutimiza yale
yaliyokusudiwa.
Mchezaji mwingine alierejeshwa
kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Wales ni kiungo wa klabu ya West Ham Utd Jack Collison ambae hakupata kuichezea
timu ya taifa lake mwaka mmoja uliopita ambapo kwa mara ya mwisho alionekana
wakati wa mchezo wa kumbu kumbu ya aliekua kocha wa timu ya taifa ya Wales Gary Speed ambae ni marehemu ambapo
Wales walicheza dhidi ya timu ya taifa ya Costa Rica.
<p>Your browser does not support iframes.</p>
0 comments:
Post a Comment