Eden Hazard
Na Shaban Kondo.Chama cha wachezaji wa kulipwa nchini Uingereza PFA, kimemkana winga kutoka nchini ubelgiji na klabu ya Chelsea Eden Hazard kufuatia sakata la kumpiga kijana anaeokota mipira katika uwanja wa Liberty Charlie Morgan wakati wa mchezo wa pili wa hatua ya nusu fainali ya kombe la ligi uliochezwa usiku wa kuamkia jana.
Chama
cha wachezaji wa kulipwa nchini Uingereza PFA, kimemkana winga huyo kupitia kwa
mtendaji wake mkuu Gordon Taylor
ambapo amesema Eden Hazard hana
mamlaka ya kujichukulia sheria mkononi, zaidi ya kuacha sheria zilizotungwa
zichukue mkondo wake juu ya sakata la kumpiga kijana muokota mipira.
Amesema tukio
hilo moja kwa moja linajidhihirisha wazi kwamba chama cha soka nchini
Uingereza kitamuadhibu mchezaji huyo kutokana na kile alichokitenda na wao kama
chama cha wachezaji wa kulipwa hawawezi kuingilia kutokana na hali halisi
kutohitaji utetezi.
Hata hivyo Gordon Taylor amesema bado wanasubiri
taarifa rasmi kutoka FA kama itawafikia na endapo watahitajika kwa ajili ya
kumtetea mchezaji huyo watajitokeza lakini wanaamini kisu cha sheria kitamkata Eden
Hazard.
Katika hatua nyingine meneja wa klabu ya Chelsea Rafael Benitez amekiri mchezaji wake alifanya makosa makubwa ya
kumpiga kijana huyo, lakini bado akaendelea kusisitiza kwamba bado suala hilo
lina wigo mpana wa kujadiliwa.
Hata hivyo
Benitez ameshauri suala hilo kutazamwa upya kutokana na kijana Charlie Morgan kuchangia kitendo
alichofanyiwa kufuatia kitendo cha kuupiga mpira kabla ya kutaka kuukota, na
hivyo kumsababishia Hazard kuamini
huenda alikua anapoteza muda kwa makusudi.
Wakati
huo huo Eden Hazard ameomba radhi
kufautia kitendo cha kumpiga Charlie
Morgan kwa kusema halikua kusudio lake kumpiga kijana huyo bali alitaka
kuupiga mpira na kwa bahati mbaya alijikuta anafanya tofauti.
Amesema
anajua jamii itayapokea maneno hayo tofauti lakini amesisitiza ukweli ndio huo
na hana lingine la kusema zaidi ya kumtaka radhi Charlie Morgan pamoja na jamii ya soka ulimwenguni kote.
Baada ya
kitendo hicho Eden Hazard
alionyeshwa kadi nyekundu huku akiiacha timu yake ikiangamia kwa kutolewa
kwenye michuano ya kombe la ligi dhidi ya Swansea ambao wametinga katika hatua
ya fainali kwa jumla ya mabao mawili kwa sifuri waliyoyapata katika mchezo wa
awali kabla ya usiku wa kuamkia jana ambapo waliambulia matokeo ya sare ya
bila kufungana.
0 comments:
Post a Comment