Chanzo;- Bomba FM Mbeya.
Mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatusi
Kinawiro amewataka wakulima kugharamia pembejeo za kilimo ambazo zipo tayari
kwa mawaka badala ya kusubiria vocha za Ruzuku.
Ameyasema hayo kufuatia kuwepo kwa
malalamiko ya wananchi wilayani Chunya kuhusu kucheleweshewa vocha za Ruzuku na
kwamba mbolea na mbegu zimepelekwa karibu na wananchi kwa hiyo wakulima
wanapaswa kwenda kununua kwa mawakala, ila ruzuku ni bado tatizo nila mbegu
zimeletwa OPV badala ya Chotara.
Amesema sehemu kubwa ya wananchi
wanamiliki mashamba yenye ukumbwa wa zaidi ya heka moja huku ruzuku ya Serikali
inatolewa kwa mkulima aliye na shamba lenye ukubwa wa heka moja kwani hutolewa
mbegu mbolea ya kupandia na kukuzia.
Aidha, ameelezea changamoto kubwa ni
kuwa ruzuku hizo zinapotolewa lakini huwa ni tofauti kwani wananchi hawazitumii
na badala yake wanaziuza na wanapaswa kuwa wawazi kwa sababu serikali
ilishawajengea kwa miaka tangu ya 2008/2009 na wananchi waliofaidika ni zaidi
ya 30000.
Kuhusu maafa yatokanayo na mvua Mkuu
huyo wa wilaya Deodatus Kinawiro amesema maafa yaliyotokea si makubwa
ukilinganisha na mwaka jana, licha ya Kata ya Mbugani nyumba kama 18
ziliezuliwa kutokana na mvua na upepo lakini anashukuru wananchi wameweza
kuezeka nyumba hizo kwa bati na wengine wamejiwekeza kwa ndugu zao lakini suala
la barabara linapotokea tatizo sehemu korofi huzirekebisha na magari kuendelea kupita.
0 comments:
Post a Comment