Jeshi
la polisi lilifika eneo la tukio na kushuhudia ng'ombe huyo akiwa
amefariki lakini hawakuchukua hatua zozote za kisheria dhidi ya
mwekezaji wa Kapunga Rice Project wilayani Mbarali aitwaye Bwana Gerry
Baquzein, aliyetumia gari lake kufanya mauaji ya ng'ombe huyo.(Picha na Maktaba yetu).
Habari kamili.
Kesi
inayowakabili wawekezaji wa Kapunga Rice Project dhidi ya wakulima wa kijiji
cha Kapunga imeendelea katika mahakamu ya mkoa Mbeya ambapo wananchi wa
kijiji jicho wameanza kutoa ushahidi wao.
Kesi
hiyo inayoendeshwa na Hakim mfawidhi wa mahakama hiyo Maiko Mteite huku
wawekezaji hao wakitete na mwanasheria wa kujitegemea Radislaus Rwekaza wakati
wakulima wao wakitete na wakili wa Serikali Achirey Mulisa ambapo kutokana na
utata wa lugha wanayoitumia watuhumiwa na walalamikaji mahakama ililazimika
kumtafuta mkarima wa lugha ya Kiingereza na Kiswahili kutoka chuo kikuu cha
sheria Mzumbe Judith Kyamba.
Asubuhi
ya leo wakulima wawili wametoa ushahidi wao ambapo wamesema kutokana na kitendo
cha mwekezaji huyo kumwagia sumu mashamba yao
yenye zaidi heka 10 wameingia hasara ya mamilioni ya fedha.
Kesi
hiyo yenye namba 43 ya mwaka 2012 imefunguliwa na wakulima hao wa Kapunga huku
wakiwatuhumu meneja wa shirika, Afisa
ughani na rubani wa Kapunga Rice Project na kwamba kesi hiyo itaendelea tena
kesho asubuhi.
0 comments:
Post a Comment