MJUMBE
wa Halmashauri kuu CCM Taifa Bw.Sambwee Sitambala
Asema yatakuwa
ya amani bila Vurugu
Asema sera
ya CCM ni kutetea wananchi
MJUMBE wa Halmashauri
kuu CCM Taifa Bw.Sambwee Sitambala anatarajiwa kuongoza
maandamano ya amani ya wananchi zaidi ya 5000 wa
mtaa wa Gombe kusini kwenda kwa mkuu wa Mkoa wa Mbeya
kwa ajili ya kupinga amri ya kutaka kuwahamisha kwenye nyumba
zao na eneo hilo kupewa watu wengine.
Akizungumza
na waandishi wa habari baada ya kwisha kwa mkutano wa wananchi hao diwani
wa Kata ya Itezi jijini Mbeya Bw.Frank Mayemba ambaye
pia ni mjumbe wa Mkutano mkuu Taifa CCM alisema kuwa
katika maandamano hayo watashirikiana na
Bw.Shitambala kuongoza hadi kufika kwa mkuu wa Mkoa.
Alisema kuwa wananchi
hao ambao zaidi ya asilimia 90 ni wanachama wa CCM walifikia hatua
hiyo baada ya kuona hawasikilizwi katika kilio chao ambacho
wamekuwa wakitoa kwa Jiji la Mbeya kuwataka kutowagusa kwa kuwa walipewa maeneo
hao kihalali baada ya kubadilishwa matumizi yake ya awali ambayo
yalikuwa viwanda.
Bw.Mayemba alisema
kuwa kutokana na hali hiyo wamedhamiria kudai haki yao kwa mkuu wa
Mkoa ambaye ndiye msimamizi wa Halmashauri zote Mkoa wa Mbeya
ambapo kutokana na hekima yake walisema kuwa wana imani kuwa
atawasaidia kuwasikiliza ombi lao na kusitisha zoezi hilo ambalo
ni athari kubwa kwa wananchi hao.
Alisema kuwa
wananchi hao baada ya kupewa viwanja hivyo wamekaa katika eneo hilo kwa
zaidi ya miaka 20 na hivyo kisheria kuwa wamiliki haklali wa
maeneo haio wasio takiwa kubughudhiwa na hivyo kushangaa wakati wote
wanapoambiwa kuwa watahamishwa na maeneo yao kupewa watu wengine.
"sisi
tunasema kama viongozi wa chama hakika
hatutakubali suala hili kwa kuwa ni wamiliki halali wa eneo
hili na hivyo kama wanataka kugawa basi tuweke mkataba ambao
watatugawia sisi na wala si wengine kama wanavyotaka kufanya
sasa hawa wataalam."alisema.
Naye
Bw.Shitambala ambaye pia ni Kaptain wa jeshi mstaafu na mwanasheria
maarufu alisema kuwa ataongoza maandamano hayo ya amani hadi kwa
mkuu wa Mkoa na hakuna vurugu itakayotokea kwa kuwa CCM
ni chama kinachohamasisha amani na utulivu na hivyo wao
wataonesha mfano.
Kada huyo wa CCM ambaye
awali alikuwa mwenyekiti wa CHADEMA kabla ya kumamia chama
hicho alisema kuwa wataomba vibali polisi kwa ajili ya kulinda maandamano
hayo na kamwe hawatachoma barabara kama wanavyofanya wengine
ambnapo watapata nafasi ya kumweleza mkuu wa Mkoa hoja
zao zinazopinga kuondolewa katika eneo hilo .
Alisema yeye kama mkazi
aliyejenga eneo hilo ni dhambi kubwa kuona wananchi wenzake na yeye
akiwemo wakinyanyaswa na hivyo kupelekea hasira kali kwa
chama hali ambayo alisema kuwa katika mkutano mkuu wa chama
na vikao mbali mbali wamekubaliana kupinga hali hiyo na
kuwapa haki yao wanachama .
Kwa hisani ya Charles Mwakipesile Mbeya
0 comments:
Post a Comment