Chama
cha wakulima AFP Leo kimekutana na tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya na
kutoa mapendekezo yao wakitaka katiba mpya ijayo itaje idadi ya wizara
zisizozidi 15 ikiwemo wizara mpya itakayoshughulika na mafuta pekee.
Katibu
Mkuu AFP Rashid Rai amesema mafuta kuwekwa wizara moja na madini siyo sawa kwa
kuwa watendaji Wanakuwa na tamaa zaidi ya kushughulikia madini kwa sababu ya
maslahi yao binafsi na si kwa maslahi ya Taifa kujikwamua kiuchumi.
Akizungumzia
suala la kuwa na Serikali moja naibu Mkurugenzi wa uenezi na habari wa chama
hicho Shaban Akwitimba amesema katiba itoe fursa kwa kiongozi kuondolewa
madarakani.
Mwenyekiti
wa chama cha NLD Dokta Emmanuel Makaidi amependekeza katiba mpya ijayo iwape
haki wananchi ya kuwa na uwezo wa kumkataa mbunge wa kuchaguliwa kutokana na udhaifu katika utendaji kazi.
Utoaji
wa maoni kwa vyama vya siasa umeanza jana kwa CCM, CHADEMA na CUF na hii leo ni
zamu ya chama cha wakulima AFP, NLD na DP na kufanya idadi ya vyama vilivyotoa
maoni yao kwa tume ya katiba mpya kufikia sita.
0 comments:
Post a Comment