Kwa hisani ya Shaban Kondo.
Wakati leo
ndiyo mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu za kuwania nafasi za uongozi wa
shirikisho la soka nchini TFF pamoja na bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPL Board) mpaka jana waliochukua fomu 36 huku wadau 18 wakizirejesha.
Afisa habari wa
shirikisho la soka nchini TFF Boniface Wambura amesema idadi hiyo ni kufikia
leo mchana lakini akasisitiza matarajio ya idadi ya wadau waliochukua fomu
kuongezeka itakapofika leo alasiri ambapo ndio itakua mwisho wa kurejesha
fomu kwa muyjibu wa utaratibu uliotangazwa na kamati ya uchaguzi.
Wakati mchakato
wa uchaguzi wa TFF ukiendelea hivyo, aliekuwa katibu mkuu wa FAT kwa sasa TFF Michael Richard Wambura amekua miongoni
mwa wadau waliojitokeza kurejesha fomu za kuwani nafasi ya umakamu wa raisi.
Wambura
amerejesha fomu hizo, huku akiwahusia waandishi wa habari jambo la kuwa
waadilifu katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi wa TFF uliopangwa
kufanyika February 24 jijini Dar es salaam.
Wakati huo huo
aliekua muamuzi mahiri Omari Abdul Kadir nae amejitosa kuchukua fomu za kuwania
nafasi ya ujumbe wa kamati ya Utendaji Kanda ya Dar es salaam.
Omari Abdul Kadir
amesema kilichomzuta hadi kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo ni kutaka
kurekebisha masuala kadha wa kadha ndani ya TFF lakini kubwa ni suala la
waamuzi ambao imefikia wakati wanaangushiwa vipondo wanapokua katika majukumu
yao.
Orodha kamili ya
waombaji ni Athuman Nyamlani, Jamal Malinzi na Omari Mussa Nkwarulo (urais)
wakati waombaji wa umakamu wa rais mpaka sasa ni Michael Wambura, Ramadhan
Nassib na Wallace Karia.
Kwa upande wa
wajumbe wa Kamati ya Utendaji na kanda zao kwenye mabano ni Salum Chama (Kagera
na Geita), Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano
(Mara na Mwanza).
Epaphra Swai na
Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo na Elly Mbise (Arusha na
Manyara), Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Blassy Kiondo,
Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama
(Njombe na Ruvuma).
Athuman Kambi na
Zafarani Damoder (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na
Singida), Farid Nahdi, Geofrey Nyange na Twahili Njoki (Morogoro na Pwani),
Elias Mwanjala na Eliud Mvella (Iringa na Mbeya), Khalid Mohamed (Kilimanjaro
na Tanga) na Muhsin Balhabou, Omari Abdulkadir na Shaffih Dauda (Dar es
Salaam).
Kwa upande wa
Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) waliochukua fomu mpaka sasa ni wawili tu. Yusuf
Manji amechukua fomu ya uenyekiti wakati Said Mohamed amechukua fomu ya kuwania
umakamu mwenyekiti.
Shirikisho
la soka nchini TFF limeendelea kusisistiza tarehe ya kuanza kwa mzunguuko wa
pili wa ligi kuu ya soka Tanzania bara kwa kuviarifu vilabu vinavyoshiriki ligi
hiyo.
Afisa habari wa
TFF Boniface Wambura amesema mzunguuko wa pili wa ligi kuu ya soka Tanzania
bara utaanza Januari 26 kama ulivyokua umepangwa lakini kuna baadhi ya michezo
itafanyiwa marekebisho kufuatia maombi ya televisheni ya SuperSport ya kutaka
kuonyesha michezo ya Super Week kama ilivyokuwa katika mzunguko wa kwanza.
0 comments:
Post a Comment