Mstahiki meya wa jiji la Mbeya Athanas Kapunga amesema
kumekua na tabia ya kuwepo msongamano wa abiria katika vituo vya
mabasi yaendayo mikoani visivyo rasmi
hasa kituo kidogo cha magari eneo la Mwanjelwa.
Akizungumza
na Bomba FM amesema kuwa halmashauri ya jiji imejipanga kushughulikia
suala hilo na wana mikakati juu ya kulijenga jiji la Mbeya.
Amesema halmashauri
ya jiji la Mbeya imedhamiria kuzirekebisha barabara zote kwa kiwango cha lami
ambapo kila mwaka halmashauri itakuwa ikijenga barabara zenye urefu wa kilometa
10.
Aidha
amesema ili kukabiliana na msongamano wa magari kati kati ya Jiji Halmashauri
imedhamiria ya kujenga vituo vya mabasi yaendayo wilayani mwanzoni mwa mji.
Kapunga amekiri kuwa utaratibu wa sasa wa mipango miji si
mzuri na halmashauri hiyo imejipanga katika mipango hiyo ikiwa na nia ya kuboresha barabara za
mitaa ili kupunguza vituo vya mabasi visivyo rasmi.
Hata hivyo amekemea vikali vitendo vya
madereva ambao wamekuwa wakitoka eneo la stendi kuu na kuifanya stendi
eneo la Mwanjelwa ambalo si rasmi kwa mabasi yaendayo mikoani.
Wakati huohuo ametoa wito kwa taasisi za kibenki kuanza kuangalia namna ya kujenga ofisi zao pembezoni mwa mji ili kurahisisha huduma kwa wananchi wanaolazimka kuja mjini kuzifuata
Wakati huohuo ametoa wito kwa taasisi za kibenki kuanza kuangalia namna ya kujenga ofisi zao pembezoni mwa mji ili kurahisisha huduma kwa wananchi wanaolazimka kuja mjini kuzifuata
0 comments:
Post a Comment