Na Shaban Kondo.
Kamati ya Sheria,
Maadili na Hadhi za Wachezaji iliyokutana Januari 19 mwaka huu chini ya
Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa
imeliondoa shauri lililokuwa mbele yake dhidi ya klabu ya Simba lililowasilishwa
na wachezaji Pascal Ochieng na Daniel Akuffo baada ya pande hizo
kufikia makubaliano.
Afisa habari wa
shirikisho la soka nchini TFF Bonifas
Wambura amesema wachezaji hao kutoka nchini Kenya na Ghana waliwasilisha
malalamiko mbele ya kamati wakipinga kukatizwa kwa mikataba yao bila kulipwa
haki stahili.
Kama itakumbukwa vyema Pascal
Ochieng anaecheza nafasi ya ulinzi alitangaza msimamo wake mwishoni mwa
mwaka jana kupitia kipindi hiki kwa kudai atahakikisha analipwa haki zake
stahiki, baada ya uongozi wa Simba kumuondoa kwenye orodha ya wachezaji
waliosajiliwa na klabu hiyo katika kipindi cha dirisha dogo la usajili.
Ochieng
alitangaza msimamo huo, baada ya kluwasilisha vielelezo vyake katika ofisi za
shirikisho la soka nchini TFF ambavyo vilikua vinainisha makubaliano
yaliyokuwepo kati yake na uongozi wa klabu ya simba uliomsajili mwanzoni mwa
msimu huu akitokea Johor FC ya nchini kwao Kenya.
Wakati huohuo Msanii wa kizazi kipya Hussein Rashid * Hussein Machozi*
ameonyeshwa kushangazwa na uteuzi wa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya
Tanzania Taifa Stars Sylvester Mash kwa kudai kocha huyo hana sifa za kutosha
katika wadhifa waliopewa.
Hussein Rashid amesema kushangazwa na uteuzi wa kocha huyo
alipohojiwa na kipindi hiki ambapo amaaleza kwamba Sylvester Mash ni kocha
ambae hakupendezwa nae wakati akicheza soka akiwa na klabu ya Kagera Sugar,
baada ya kuona alidhamiria kukiua kipaji chake ambacho kilikua chanzo cha
kusajiliwa na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya soka Tanzania bara.
0 comments:
Post a Comment