Mkuu
wa wilaya ya Mbeya Dakta Norman Sigala ameitaka jamii kuendelea kuchangia
shughuli za kimaendeleo katika elimu ili kuwawezesha wanafunzi kuanza elimu ya
Sekondari kwa wakati.
Ameyasema
hayo leo katika mkutano wa hadhara wenye lengo la kuhamasisha maendeleo ya
elimu katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya vijijini amesema wazazi wanapaswa
kuchangia maendeleo, na walimu wakishatengenezewa mazingira mazuri ya
kufundisha hakuna mwali ambaye anakuwa mvivu.
Aidha
amewataka wanafunzi wa shule ya Sekondari Usongwe kuwa na nidhamu masomoni ili
waweze kufikia malengo waliyoyakusudia na kufikia Januari 30 mwaka huu vyumba
vya madarasa katika shule hiyo vitakuwa vimekamilika ili kutoa furasa kwa
wanafunzi kusoma kwa uhuru.
Dakta
Sigala ametoa pongezi kwa wananchi waliowekeza katika kuchangia maendeleo ya
elimu na amewaagiza wananchi hao kuwafahamisha wananchi wenzao kuwa hakuna
elimu bora inayopatikana bila kuchangia kwa hiyo hawana budi kukata tama ya
kutoa michango pindi wanapohitajika kuchangia.
Kwa
upande wao waalimu wa shule hiyo wameiomba Serikali kuangalia namna ya
kupunguza makato kwa waalimu ili kuwawezesha kuwa na kipato kikubwa kitakachowawezesha
kujikimu kimaisha.
0 comments:
Post a Comment