Pages


Home » » SHIRIKISHO la Soka barani Afrika-CAF limelitoza faini ya dola 10,000 Shirikisho la Soka la Ethiopia .

SHIRIKISHO la Soka barani Afrika-CAF limelitoza faini ya dola 10,000 Shirikisho la Soka la Ethiopia .

Kamanga na Matukio | 01:25 | 0 comments

AFCON_2013-NA_KABUMBU_LIANZE

SHIRIKISHO la Soka barani Afrika-CAF limelitoza faini ya dola 10,000 Shirikisho la Soka la Ethiopia baada ya mashabiki wake kutupa mavuvuzela pamoja na chupa za maji uwanjani wakati wa mchezo wao dhidi ya Zambia ambao walitoka sare ya bao 1-1 Jumatatu.

CAF ilitangaza kuwa nusu ya adhabu hiyo ya dola 10,000 itasamehewa kama tu mashabiki wa Ethiopia hawatarudia tukio hilo katika kipindi chote cha mashindano.

Ethiopia inayoshiriki michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon kwa mara ya kwanza baada ya miaka 31 ina mashabiki wengi waliokuja kuiunga mkono timu yao lakini mchezo wao wa kwanza uliochezwa katika Uwanja wa Mbombela uliingia dosari baada ya mwamuzi Eric Otogo-Castane alipompa kadi nyekundu golikipa Jemal Tassew muda mchache kabla ya mapumziko.

Mara baada ya mwamuzi huyo kutoa kadi vuvuzela na chupa za maji zilimiminika uwanjani zikitokea jukwaani huku makocha na wachezaji wa akiba wakijificha wasiumizwe na vitu hivyo wakati mtangazaji uwanjani hapo alikiwaomba mashabiki hao kutulia.

Mashabiki hao wa Ethiopia pia wanaweza kufungiwa kuingia uwanjani katika mchezo wa Ijumaa dhidi ya Burkina Faso labda CAF ipate uhakika kutoka EFF kuwa watawadhibiti mashabiki wao.

 Wakati huo huo WENYEJI wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, Afrika Kusini, maarufu kama Bafana Bafana, leo wamefanikiwa kujiwekea mazingira mazuri ya kuingia Robo Fainali baada ya kuichapa Angola Bao 2-0 katika Mechi ya Kundi A iliyochezwa Uwanja wa Moses Mabhida huko Jijini Durban.

Huu ni ushindi wa kwanza kwa Bafana Bafana baada ya kutoka sare na Cape Verde katika Mechi ya ufunguzi.

+++++++++++++++

MAGOLI:

South Africa 2

-Siyabonga Sangweni Dakika ya 30

-Lehlohonolo Majoro 62

Angola 0

+++++++++++++++

Aliewapa Bafana Bafana Bao lao la kwanza ni Senta hafu Siyabonga Sangweni katika Kipindi cha Kwanza na Lehlohonolo Majoro kupiga la pili Kipindi cha Pili.

Baadae leo itakuwepo Mechi ya pili ya Kundi A kati ya Morocco na Cape Verde ambayo pia itachezwa Uwanja wa Moses Mabhida huko Mjini Durban.

VIKOSI:

South Africa: Khune, Ngcongca, Khumalo, Sangweni, Masilela, Mahlangu, Furman, Phala, Parker, Mphela, Rantie

Akiba: Sandilands, Gaxa, Nthethe, Majoro, Tshabalala, Serero, Matlaba, Letsholonyane, Manyisa, Meyiwa.

Angola: Lama, Airosa, Dany Massunguna, Miguel, Bastos, Pirolito, Mateus, Dede, Geraldo, Guilherme, Manucho

Akiba: Landu, Lunguinha, Fabricio, Djalma, Manucho Dias, Zuela, Gilberto, Amaro, Yano, Mingo Bile, Manuel, Neblu.

Refa: Koman Coulibaly (Mali)

Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger