Chanzo Bomba FM Mbeya 104,0MHz
Taasisi
ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Mbeya imewakamata na kuwafikisha mahakama ya Wilaya ya Rungwe, hakimu wa
mahakama ya mwanzo ya Kata ya Lupata Andrew Siwale na afisa mtendaji wa kata ya
Kisegese Gasper Bagomoke kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa pamoja na
vitendo vya uonevu hasa kwa watu wasio na kipato.
Wakiongea
na Bomba FM wananchi wa eneo husika wamesema watendaji wa kata hiyo wamekuwa
wakimtoza faini mwananchi hadi shilingi laki tatu kwa kosa moja na kuteswa kwa
mwananchi asiyekuwa na kipato cha kutosha cha kulipia faini.
Kwa
upande wake afisa mtendaji wa kata hiyo Bwana Bagomoke amekiri kuwa hakimu huyo
kuchukuwa fedha kwa watuhumiwa wanaobainika na makosa mbalimbali na kuwaagiza Migambo
kuwanyanyasa wananchi pamoja kuwatoza faini kwa kuwapandikizia kesi.
Aidha,
akiongelea sakata hilo Mkuu wa Taasisi ya hiyo mkoani hapa Daniel Mtuka amesema
viongozi hao wamekamatwa January 15 katika maeneo mawili tofauti mmoja akiwa
Kata ya Kisegese na mwingine kata ya Itete na kasha kuhojiana nao na kupata
ushahidi.
Amesema
viongozi hao waliunda mahakama yao kinyume cha kanuni za Serikali ambapo kesi
zao zilikuwa zikiendeshwa nyakati za jioni na usiku na kesi kuanzia saa 12 kusikilizwa
kukiwa hakuna karatasi zozote zinazohusikana na mahakama, bendera, picha za
viongozi na risiti za faini na wakati mwingine kama jingo likiwa na tatizo la
umeme ukikatika vibatali vilikuwa vikiwashwa ili kesi iweze kumalizika.
Mtauka
amesema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kwa kifungu namba 15 kifungu
kidogo cha kwanza na cha pili cha mwaka 2007, cha sheria ya kuzuia na kupambana
na rushwa cha kuomba na kupokea rushwa, ambapo mlalamikaji aliomba rushwa ya
shilingi laki mbili kufuatia kesi ya awali ya msingi ya kwa wizi na kuharibu
mali kati ya Bi Elizabeth Mlenga na mlalamikaji.
Wakati
huohuo TAKUKURU imejipanga kikamilifu katika kukomesha vitendo vya uonevu
vinavyofanywa na watendaji wa Serikali katika mahakama ya mwanzo na mabaraza ya
kata ili haki ya msingi kupatikana kwa maslahi ya wananchi na viongozi.
Hata
hivyo kuhusu faini anayotakiwa kutozwa mwananchi katika mabaraza ya kata Mkuu
wa mkoa wa Mbeya Abasi Kandoro amewataka viongozi wa mabaraza hayo kutomtoza
mwananchi kiasi kikichozidi shilingi elfu kumi.
0 comments:
Post a Comment