Pages


Home » » TFF, leo inatarajia kufungua milango kwa wadau wa michezo, kwa ajili ya kuwasilisha pingamizi dhidi ya wagombea.

TFF, leo inatarajia kufungua milango kwa wadau wa michezo, kwa ajili ya kuwasilisha pingamizi dhidi ya wagombea.

Kamanga na Matukio | 03:00 | 0 comments



Na Shaban Kondo.
Kamati ya uchaguzi ya shirikisho la soka nchini TFF, leo inatarajia kufungua milango kwa wadau wa michezo, kwa ajili ya kuwasilisha pingamizi dhidi ya wagombea waliopitishwa kwa ajili ya kuwania nafasi mbali mbali za uongozi wa shirikisho hilo.

Afisa habari wa TFF Bonifas Wambura amesema kamati hiyo iliyo chini ya mwenyekiti Deogratius Lyato, itafungua milango hiyo kwa wadau, baada ya kupitia fomu za wagombea zilizorejeshwa kwa wakati pamoja na kuhakikisha vielelezo vilivyoambatabnishwa katika fomu hizo.

Majina yaliyopitishwa na kamati ya uchaguzi kwa ajili ya kuwani nafasi za uongozi wa TFF upande wa raisi ni Athuman Nyamlani, Jamal Malinzi, na Omari Nkwarulo.

Makamu wa Rais Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia .

Kwa upande wa ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Abdallah Musa, Salum Chama na Kaliro Samson (Kagera na Geita), Jumbe Magati, Mugisha Galibona, Richard Rukambura, Samuel Nyalla na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).

Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo, Elly Mbise na Omari Walii (Arusha na Manyara), Ahmed Mgoyi na Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Blassy Kiondo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama na Stanley Lugenge (Njombe na Ruvuma).

Athuman Kambi, Francis Ndulane na Zafarani Damoder (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi, Hassan Othman Hassanoo, Riziki Majala na Twahili Njoki (Morogoro na Pwani), David Lugenge, Elias Mwanjala, Eliud Mvella na John Kiteve (Iringa na Mbeya), Davis Mosha, Khalid Mohamed na Kusiaga Kiata (Kilimanjaro na Tanga) na Alex Kamuzelya, Juma Pinto, Muhsin Balhabou, Omari Abdulkadir na Shaffih Dauda (Dar es Salaam).


Kamati ya uchaguzi limeliondoa jina la Richard Julius Rukambura; baada ya kubaini muombaji alivunja kanuni za Uchaguzi  za TFF Ibara ya 10(8) kwa kuomba nafasi  mbili za Rais na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kwenye uchaguzi  wa TFF.

(mwingine alioondolewa katika uchaguzi huo ni Titus Osoro ambae amethibitisha kujitoa kugombea nafasi ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF.

Wakati mchakato wa uchaguzi wa TFF ukiendelea, wanamichezo wa mkoani mwanza wameonyesha kuchukizwa na mjumbe wa kati ya utendaji ya TFF anaetetea nafasi yake Samuel Nyalla kuwa mstari wa mbele katika harakati za kupoozesha michezo mkoani humo.

Akizungumza kwa niaba ya wanamichezo wa mkoani Mwanza katibu mkuu wa chama cha makocha wa soka mkoani humop TAFCA Abubakari Said Behengula amesema Samuel Nyalla hakustahili kuweka dhamira ya kurejea katika madaraka ya soka kupitia TFF kutokana na mengi mabaya anayoyafanya.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger