Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akitoa maelekezo kwa Waziri wa Ujenzi Dkt John
Pombe Magufuli, Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe na Waziri wa
Fedha Dkt William Mgimwa kabla hajahutubia Jumatatu mkutano mkubwa wa
hadhara mjini Nzega katika ziara yake ya siku nne ya mkoa wa Tabora
ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na
maji.
(PICHA NA IKULU)
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisikiliza maelezo ya Meneja wa TANESCO wa Nzega
akielezea mikakati ya kuwapatia wakazi wa hapo nishati hiyo
Jumatatu mkutano mkubwa wa hadhara mjini Nzega katika ziara yake ya siku
nne ya mkoa wa Tabora ambapo anazindua miradi kadhaa ya maendeleo
ikiwemo barabara, daraja na maji.
Umati wa wananchi ukiwa katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Rais Jakaya Kikwete mkoani Tabora leo
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ripoti ya maendeleo ya Wilaya ya Uyui
toka kwa mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Lucy Mayenga wakati Rais alipowasili
Tabora mjini kuendelea na ziara yake ya siku nne ya mkoa wa huo ambapo
anazindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo barabara, daraja na maji.
Habari Kamili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya
Kikwete amekerwa na utendaji kazi mbovu wa mkurugenzi wa halmashari ya Nzega
mkoani Tabora, baada ya mkurugenzi huyo kushindwa kuwapatia wananchi wake
huduma ya maji safi.
Awali akiongea kwenye mkutano huo wa
hadhara mbunge wa jimbo la Nzega Hamisi Kigangwala amesema pamoja na vikao vya
halmashauri kutoa kipaumbele katika mradi wa maji bado mkurugenzi huyo amekuwa
akiukataa.
Naye waziri wa maji Profesa Jumanne
Maghembe amesema kitendo cha halmashauri hiyo kukosa maji ni cha aibu ambapo
amesema kwa nafasi aliyonayo mhandisi wa maji wilayani humo lazima awajibishwe.
Akiongea huku akionekana mtu
aliyesikitishwa kusikia wananchi wake wakikosa maji safi na salama licha ya
kuwepo kwa mipango mingi ya kuboresha huduma hiyo Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dokta Kikwete amesema hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya
mkurugenzi huku akiwaahidi wananchi hao huduma ya maji safi na salama.
0 comments:
Post a Comment