Na Shaban Kondo.
Wadhamini
wa ligi kuu ya soka Tanzani bara wametangaza kuwa tayari kwa kipyenga cha
mzunguko wa pili wa ligi hiyo kitakachopulizwa kuanzia Januari 26 mwaka huu.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam, Meneja Mahusiano ya Nje wa Kampuni
ya Vodacom inayodhamini ligi kuu, Salum Mwalim amesema kwamba kampuni yake
inajisikia fahari kuona soka sasa inachezwa viwanjani zaidi na si nje hivyo
wanatarajia upinzani mkubwa katika mzunguuko wa pili.
Salum Mwalim
pia akatoa shukurani kwa TFF pamoja na kwa kamati ya Ligi kufautia ushirikiano
mzuri wanaowaonyesha, katika kuendeleza na kuleta chachu ya ligi kuu ya soka Tanzania
bara ambayo mwanzoni mwa msimu huu ilianza kwa changamoto kadha wa kadha.
Wakati huo
huo shirikisho la soka nchini TFF kupitai kwa Afisa habari Bonifas Wambura
limetoa kauli ya kuwa tayari kwa kipyenga cha mzunguko wa pili, kupulizwa baada
ya kukamilisha maandalizi yote yanayostahili.
Michezo
ya ligi kuu itakayochezwa mwishoni mwa juma hili ni kati ya;
African
Lyon
|
-
|
SIMBA
Sports Club
|
Mtibwa
Sugar
|
-
|
Police
Morogoro
|
Coastal
Union
|
-
|
Mgambo
JKT
|
Ruvu
Shooting
|
-
|
JKT
Ruvu
|
Azam
|
-
|
Kagera
Sugar
|
JKT
Oljoro
|
-
|
Toto
Africans
|
Wakati matayarisho ya mzunguuko wa pili wa ligi kuu msimu huu yakiwa
katika mstari wa mafanikio kwa mara
ya kwanza wadhamini wa
ligi hiyo kwa kushirikiana na kampuni ya LAJANN
E-SYSTEMS ENTERPRISE wamezindua tovuti maalum itakatohusika na ligi kuu.
Daniel
Mwakamele msemaji wa msemaji wa Kampuni ya
LAJANN amesema wamefanikisha uzinduzi huo baada ya kufanya kazi kwa umakini
huku wakiamini kila mtanzani watakua akipata taarifa za ligi kwa wakati na kwa
umakini.
0 comments:
Post a Comment