Mbeya.
Wadau mbalimbali walioahidi kutoa msaada
kwa familia ya Daudi Mwangosi wamekumbushwa kutekeleza ahadi zao ili kuiwezesha
familia hiyo kujimudu kimaisha.
Rai hiyo imetolewa na mkurugenzi wa umoja
wa vilabu vya waandishi wa habari nchini (UTPC) Abubakar Karsan wakati akiongea
na waandishi wa habari mkoani hapa.
Amesema licha ya ahadi mbalimbali
zilizotolewa na baadhi ya wafanyabiashara na wanasiasa hakuna ahadi hata moja
ambayo imetekelezeka hadi sasa.
Wakati huohuo amesema tume iliyoundwa kwa
ajili ya uchunguzi wa kifo cha Daudi Mwangosi kilichotokea Septemba pili mwaka
jana imemaliza kazi yake na kutoa mapendekezo kwa viongozi wa jeshi la polisi
waliohusika katika oparesheni hiyo iliyopelekea kuuawa kwa Mwangosi waweze
kuwajibika.
Hata hivyo amesema umoja wa vilabu vya
waandishi wa habari nchini unatarajia kumuanzishi mradi wa ufugaji kuku wa
kisasa mjane wa Mwangosi ili aweze kuilea vyema familia yake.
0 comments:
Post a Comment