Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Sakata
la Kifo cha Mzee Nongwa Hussein Mkazi wa Kijiji cha Kalungu, Kata ya
Ivuna, Tarafa ya Kamsamba, Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya, kilichotokea
Januari 13 mwaka huu majira ya saa 10 jioni hali iliyopelekea vijana
wenye hasira kali kuhusisha kifo hicho na imani za kishirikina na
kupelekea watu wawili kati ya watatu kuzikwa hai.
Walioshutumiwa
na kuhusika na kifo hicho kwa imani za kishirikina ni pamoja na kaka wa
marehemu Bwana George Hussein, Ernest Molela na Bi. Miziana Nachela
wote wakazi wa kijiji hicho.
Wakati
mazishi yakiendelea baada ya kuchonga jeneza la marehemu vijana hao
walianza kumtafuta kaka wa marehemu huyo ambaye alifanikiwa kutoroka
kusikojulikana, na baadae kufanikiwa kuwakamata Bwana Molela na Bi.
Nachela na kisha kuanza kuwaporomoshea kipigo na kuwazika hai katika
kabuli moja na marehemu Nongwa na hivyo kuzikwa watu watatu katika
kaburi moja.
Baada
ya sakata hilo vijana hao waliondoka makaburini na taarifa kumfikia
Afisa Mtendaji wa Kata hiyo Bwana Joseph Silwimba Mengwa, ambaye alifika
eneo la tukio na kukuta kitendo hicho cha kikatili kimekwisha tendeka
na yeye kuchukua jukumu la kulitaarifu Jeshi la Polisi ambao siku ya
pili Januari 14 mwaka huu majira ya saa tatu asubuhi lilifika eneo la
tukio na kuifukua miili hiyo ya watu waliozikwa hai.
Aidha,
miili hiyo ilikabidhiwa kwa wanandugu ili kuzikwa upya katika makaburi
mengine huku wakiuacha mwili wa marehemu Nongwa katika kabuli la awali.
Uchunguzi
wa awali umeonesha kuwa baadhi ya vijana waliohusika na tukio hilo
wanashikiliwa na Jeshi la Polisi na wakati wowote mara baada ya
upelelezi kukamilika watafikishwa mahakamani.
Hata
hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoani hamo Diwani Athuman amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na amewataka wananchi kutojichukulia sheria
mikononi.
0 comments:
Post a Comment