Pages


Home » » Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Mbeya Dokta Mery Mwanjelwa ametoa msaada wa baiskeli 10 kwa walemavu wa miguu

Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Mbeya Dokta Mery Mwanjelwa ametoa msaada wa baiskeli 10 kwa walemavu wa miguu

Kamanga na Matukio | 02:45 | 0 comments
Mimi ni nani mbelezako bwana mpaka ukanijalia kuwa hai hadi hii leo nakushukuru mungu kuniokoa katika majanga mbalimbali ya mwaka uliyopita hasa kwenye ile ajali iliyonitokea Mbalizi kwani zaidi ya watu 12 walifariki hayo ni baadhi ya maneno aliyokuwa akitamka Dr Mary Mwanjelwa kwenye ibada ya shukrani iliyofanyika katika kanisa la Moravian ushirika wa Ruanda jijini Mbeya(Picha na Mwaisango)


Na Mwandishi wetu.
 Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Mbeya Dokta Mery Mwanjelwa ametoa msaada wa baiskeli 10 kwa walemavu wa miguu ikiwa ni moja ya shukrani zake kwa mwenyezi Mungu kumwokoa katika ajali ya gari mwaka jana.



Msaada huo ameutoa mara baada ya kumalizika kwa misa katika kanisa la Moroviani jimbo la kusini magharibi usharika wa Ruanda ambapo misa hiyo iliendeshwa na askafu wa jimbo hilo Alinekisa Cheyo.



Akitoa msaada huo Dokta Mwanjelwa ameiasa jamii kuwajali na kuwathamini walemavu kwa sababu ni binadamu kama tulivyo binadamu wengine na kufanya hivyo italeta chachu kwa walemavu hao kutambua kuwa mbunge wao kawakumbuka.



Naye askofu Alinikisa Cheyo amempongeza Mbunge huyo wa viti maalumu kupitia chama cha Mapinduzi Dokta Mwanjelwa kwa kuwa na moyo wa ukarimu na kwamba jambo alilolifanya ni la heshima na mwanajamii wenye uwezo wanapaswa kuwasaidia kutokana na kutojiweza kutoka sehemu mmoja na kwenda nyingine.
Share this article :

0 comments:

 
Support : Creating Website | Greyson Salufu Template | Chimbuko Letu Inc
Copyright © 2011. Kamanga na Matukio - All Rights Reserved
Template Modify by Chimbuko Letu Inc
Proudly powered by Blogger